Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Naandika nikiwa na mshangao mkubwa.
Makonda ulianzisha sintofahamu nchini kwa kusimama mbele ya hadhara ya nchi na kulitangazia Taifa kuwa Rais anatukanwa mitandaoni, na wanaomtukana rais ni wateule wake yeye mwenyewe wakiwemo mawaziri wake.
Kitendo hicho peke yake kikamdhalilisha sana rais mara tatu.
1. Mosi kwamba anadaharauliwa na wateule wake mwenyewe
2. Pili kwamba hana maamuzi ya kushughulikia utovu wa nidhamu kwa wanaovunja heshima ya mkuu wa nchi
3. Tatu, kuwafanya wananchi wafuatilie mitandaoni kujua rais katukanajwe ili "wajue". Na hii ikamvunjia heshima zaidi rais baada ya kujua kile anachotukaniwa.
Sasa hivi karibuni, umefanya ujinga mwingine, kwa kiburi na jeuri umekuwa ukizodoa, ukitoa kauli za yodo, dharau na kejeli kwa watumishi wa umma chini ya ofisi yako hadi ukaenda kufanya unyanyasaji wa kijinsia kupitia kauli. Kitendo hicho kimekemewa na wananchi badala ujitafakari uone umekosea wapi Unarudi kulekule katika KUTUMIA JINA LA RAIS kujifichia ujinga wako!.
Kitendo chako cha kurejearejea KUTUKANWA RAIS kunawafanya watu wafuatilie zaidi na zaidi vile alivyotukanwa na matokeo yake matusi kwa rais yanaenea zaidi badala ya kukoma. Na heshima ya rais inashuka!. Wengi walienda kutembelea mtandao wa yule dada baada ya mtonyo wako!
Sasa ni jukumu la Rais kuleta urafiki katika kazi kwa kukuacha ili uendelee kufanya ujinga na yeye adharaulike zaidi, au akutoe hapo ukajifunze upya maana ya kuwa mnyenyekevu.
Makonda utajifunza lini?