Makonda wa mabasi ya mikoani, kwanini mnahatarisha maisha yenu kwa kusimama karibu na kioo cha gari?

Kwenye page za mabus huwa napita nikikuta wamepiga picha pale mlangoni huwa lazima nicomment kuwa hiyo siyo sehemu nzuri wala salama kusimama lakini hao wataalam huwa wananishambulia sana, hiyo sehemu huwa naichukia sana kuona mtu hapo maana mwaka 2022 maeneo ya Vyeyula Dodoma niliwahi kushuhudia ajali iliyoua watu 9 hapohapo wengi walikua ma agent na kondkta pia alifariki.

Sasa hadi leo huwa nikisafiri na bus nikiona mtu amesimama hapo huwa natamani nimfate kumwambia atoke hapo ila wanapapenda na ni wabishi vibaya sana, japokua ajali inatokea upande wowote ila fatal risk ipo hapo sana
 
Sio kondakta tu,hata abiria usiwe Fala,unapokata kiketi epuka siti za mbele hasa kushoto mwa dereva.
Hata ukiwa na gari yako binafsi ukiwa na safari mke na watoto wakae nyuma
 
Kama unawaambia na wanabisha basi yakiwakuta ndyo watajifunza, alafu hakuna watu wajuaji kama Makonda.
 
Sio kondakta tu,hata abiria usiwe Fala,unapokata kiketi epuka siti za mbele hasa kushoto mwa dereva.
Hata ukiwa na gari yako binafsi ukiwa na safari mke na watoto wakae nyuma
Vyema sana mkuu, nimejifunza kitu hapo
 
Utawasikia kwenye kipaza..abiria mnakumbushwa kufunga mkanda kwa ajili ya usalama wenu..wakati wao ndo watu pekee kwenye basi hawafungi mkanda na wanakaa sehemu hatari
Hatari hii
 
Tatizo kubwa nipale kila anaye kuwa kwenye ofisi yake anataka kujionyesha yeye ni nani . Hata umwambie kuwa kuna hatari hapo hawezi kukuelewa.
 
Ukipewa Abood/Shabiby devera uwe wewe uweke na kutoa mizigo kwenye buti, utatoboa?
Tutafika huko tu japo siyo sasa, na hao madereva wataweza japo sasa hivi ni vigumu kwa sababu mabasi hayana tofauti na malori kwa kubeba mzigo. Hata wapiga debe watakuja kufa kifo cha mende.
 
Wengine baada ya kuuza ile seat yao, hulala pale kwenye engine..tena fofofo kabisa...Matajiri wa mabasi hebu jaribuni kujali wafanyakazi wenu
 
Iyo iko wazi mkuu ata kama ww ndio ungekuwa dereva wa hilo basi ungefanya kama alivyo fanya bwana dereva apo.
Hapo hajampelekea ila ndiyo upande aliokuwa ana-overtake nao. Hili suala la kusema dereva anakwesha upande wake mara nyingi huwa ni porojo tu.
 
inilaaah walayih rajuni hakika amekufa na utamu wake.

siyo mwarabu mimi. ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…