Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, amewataka waandishi wa habari kutumia fursa ya mahojiano naye kuuliza maswali magumu na yenye tija badala ya maswali mepesi, akisisitiza kuwa lengo ni kutoa majibu yatakayomwezesha mwananchi wa kawaida kuelewa kwa kina masuala yanayojadiliwa.
Makonda amewatoa hofu wanahabari hao kwa kuwahakikishia kuwa hatatilia maanani masuala ya umiliki wa ithibati au vitambulisho rasmi vya kazi wakati wa kuuliza maswali yao, bali anazingatia zaidi ubora na uzito wa maswali yanayohusu maendeleo ya sekta hiyo na taifa kwa ujumla.