Aisee yaani wewe ni kama mimi. Nilikuwa nakula sana kongoro lakini siku moja nikasogea kwa jamaa anayeandaa kwa kweli niliondoka bila kumtaarifu. Jamaa kwenye vidole kumejaa fungus halafu mbichi kama madonga, nilipouliza nikaambiwa asilimia kubwa ya wauzaji wa supu ya kongoro wengi wana fungus. Halafu muda mwingine unamuona anayekuandalia anachokonoa meno yake na toothpick then anashika kongoro lako.
Suala lingine ni kwenye supu za nyama au utumbo, kwenye bar za kawaida ni jambo la kawaida SUPU YAKO KUCHANGANYWA NA SUPU ALIYOBAKIZA MTEJE MWINGINE, IKIWA NI PAMOJA NA KUPEWA CHOMBO AU KIJIKO KISICHOOSHWA. NIMEYASHUHUDIA SANA HAYA MIMI BINAFSI HADI NIKAWA NINAKWENDA UMBALI MREFU KUFUATA SUPU KWA JAMAA ANGALAU ANAYEZINGATIA USAFI