Makongoro Nyerere jifunze kutoka kwa Chalamila, punguza Masihara

Kama nakumbuka vizuri, Rais SSH aliwahi kusema, bango moja tu kwenye mkutano kiongozi anaondoka madarakani.... Sasa huyu kama kasema mabango ruksa basi alikuwa anapima kina cha maji. Matokeo ni kina kirefu.
 
Albert Chalamila hajatambuliwa kwa unachodai ila kuna ' Madudu ' yake fulani aliyafanya alipokuwa RC Mbeya ambayo yalifichwa na Mtendaji Mmoja ila kuna Msagaji Kunguni Mmoja kutoka ' Makao Obey ' akayaibua na Kumwonyesha Mama kuwa ( Jamaa ) ni Mtu ' Hatari ' na atakuja ' Kumgharimu ' mbele ya Safari hivyo ni bora amuwahi tu mapema Kumuondoa.

Kuhusu Kaka yangu ( Kiukoo ) huko ' Uzanakini ' Kwetu Makongoro Nyerere kuwa apunguze ' Masihahara ' yake kwakuwa ' yatamgharimu kwa ' Mama ' nakupinga tena 100% kwani hakuna ndani ya CCM ( ambayo ndiyo inaunda Serikali ) ya Rais Samia asiyemjua Makongoro Nyerere ila Uzuri wake ( Makongoro ) anajua sana Kutenganisha muda wa Mzaha na Kazi vinginevyo CCM ' inayojitambua ' isingeweza Kumteua katika Kamati na Sekretarieti Muhimu, Nyeti na za Kimaamuzi ndani ya Chama.

Udhaifu wake mkubwa ni Bia na Maku.
 
Makongoro Nyerere ni mtu wa mizaha mizaha tangu utoto na ujana wake, kumwambia achane na hulka yake kujenga taswira isiyokuwa yake nadhani atageuka kuwa msanii tu. ... Aidha asipewe uongozi au akipewa aliyemchagua amwelewe hivyo......kwani alipokuwa mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la EAC alishindwa kuyamudu majukumu aliyopewa?.
 
Waacheni watu wawe huru kuishi Maisha yanayo wapendeza huku wakitumikia watanzania. Mteuzi hakioni hafurahi basi atengue.

Yanini kufanya kazi kwa maigizo?.
 
Waache kuabudu teuzi that is the right sentence to use. Mbona sisi tunaendelea kuishi na hatuko kwenye teuzi bana?
 
Makongoro ndivyo alivyo, hata kwenye vijiwe yuko hivyo hivyo....hanaga mambo ya ukuda

Sijui nikuweke ndani, kufokea watu

Mpka sasa wafanyakazi huko manyara wanamkubali sana

Ova

Kwa kiongozi aina ya makongoro kazi manyara itafanyika na atafanya kazi kwa raha maana atapata taarifa nyingi za mkoa wake, mwanzo nilimuona anazingua kumbe jamaa yuko poa sana
 
Duniani lazima kufanya kiasi kila kitu. Huyu mjinga alimaanisha kabisa!!! Ina maana yeye kwa kupima kwake alikuwa anaona ni sawa kutania kuwa watu wabebe mabango ya matusi? Wangebeba ya kumtukana mama ingekuwaje? Nadhani alikuwa hajui kama yeye hapo mkoani anamuwakilisha raisi wa jamhuri. Alizoea kuongea ovyo enzi za kale akadhani hata sasa atapeta kwa kuongea ovyo. Inawezekana alikasirika maana mama wakati anamuapisha alimuonya kuhusu kupiga watu. Kwa hiyo akaona amfanyizie kwa watu kwenda na mabango ya matusi!! Fala sana hili jamaa. Kwanza kachelewa sana kutumbuliwa halina hekima kabisa!!!!
 
Mako tabia ya mzaha kupita kiasi imemgharimu hadi hapa. Mi naamini ni mtu mzalendo na anachukia rushwa kama baba yake. Anahitaji kutune hapo kwenye utani na mizaha bila shaka atakua mtendaji bora
 
Mako tabia ya mzaha kupita kiasi imemgharimu hadi hapa. Mi naamini ni mtu mzalendo na anachukia rushwa kama baba yake. Anahitaji kutune hapo kwenye utani na mizaha bila shaka atakua mtendaji bora
Yeah, Mako angekuwa siyo mtu wa mizaha angekuwa ameshaaminiwa zaidi na hata Wazee waliopita, na angeweza kuwa ameshafika mbali.

Sasa ile ya kofia hoyee
Kifimbo hoyee

Na kauli za hivyo, zinachekesha ndiyo, lakini zikizidi watu wanaona hauko serius kupewa dhamana kubwa
 
Naona mleta mada,humjui vzr makongoro,Kama ulimsikiliza vzr siku anaapishwa nadhani Wala usingesumbuka ,kumpa kauahuri haka.yule akiamini hii ndio sahh,hacheleweshi anakupa laivu bila kumunya maneno.muulize jk atakwambia makongoro ni nani.
 
Muacheni huyu mzee hana shida na mtu yuko poa sn, wakati mwingine kunyenyekea sn napo ni upumbavu tupu.
True aisee ivi vyeo sijui hata watu wanavitaka vya Nini aisee unaishi unamuogopa mtu kuliko hata mungu aliekuumba.upumbavu mtupu
 
True say aisee Bora utolewe kuliko kuishi maisha ya Namna iyo ushindwe kufurai maisha kwa sababu ya TEUZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…