Makongoro Nyerere jifunze kutoka kwa Chalamila, punguza Masihara

Muone Mataga anajipa moyo! Mkija kushtuka, mtajikuta wote mko barabarani mnauza madafu! Kama ulikua hujui, huu ndiyo ukweli mchungu! Samia ni JK! Na wala siyo Magufuli kama unavyo ota.

Magufuli wako aliwapiga zengwe akina Amos Makala na Batilda Burhan (Team JK), Mama kawarudisha kundini! Halafu hao Team Magufuli wenzako ndiyo anawatumbua tu mmoja baada ya mwingine! Kuanzia Bashiru Ali, Sabaya, Chalamila! List bado inaendelea! Mpaka Mataga wote muishe!
Sawa endelea kushangilia mkuu.
 
Wewe inaonekana kumhurumia Moko kuliko wewe mwenyewe unavyotakiwa ujiurumie
 
Brother Mako

Najua wewe ni mtu wa masihara na utani utani mwiiingi. Utani hoye!

Najua wewe ndivyo ulivyo toka long time kitambo.

Ila nataka nikueleze kitu, Kuwa makini sana na utani wako usifikie hatua ya kuharibu haiba na taswira ya taasisi ya Urais au rais mwenyewe!. Namaanisha ukimtaja rais mtaje si katika muktadha wa masihara masihara, bali mtaje ukiwa serious na kwa vitu serious. Kama unataka kumtania rais basi acha hiyo kazi aliyokuteua, njoo JF tumtanie na tumchane kwelikweli akizingua!

Chalamila leo katumbuliwa, naamini sababu kubwa haswa ni ile clip aliyosikika akisema kuwa kwenye ziara ya rais huko Mwanza watu wanaweza kubeba mabango yoyote yale hata kama ni matusi! Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!

Ukizingatia kuwa clip ya Chalamila imekatwa, watu wanaweza kushindwa kujua nini logic ya kauli yake. Hata hivyo Chalamila naye ameshindwa kutumia busara kwa kushindwa kujua kuwa kauli yake inaweza kutafsirika vibaya kuwa

1. Anacheza shere agizo la rais la kuruhusu watu kubeba mabango kwenye ziara zake.

2. Kwamba anamchukulia poa rais kwa kutoa kauli za mizahamizaha

Sasa ndugu Mako, kuwa Makini na mizahamizaha hasa juu ya maagizo ya rais. Mzaha ni bora uende vizuri ila ukienda vibaya, na wabaya wako wakaikatakata clip yako ili kukuchongea, hutaeleweka vizuri.

Nakushauri ndugu Mako, Fanya Mzaha 1% ila piga kazi 99%. Na mzaha wako usiinvolve jina la rais kabisa kwa sababu ukikosea pale utapata tabu sana.

Kumbuka busara za bungeni kwa nini kuna kanuni ya kutolitumia jina la rais kwa njia za mizaha ili kujipatia uhalali wa hoja.
Nia yako ni kumtetea huyo clown. La Makongoro ni mengineyo
 
Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!
exactly, nami nimeandika hivyi twita mchana huu! Uko sahihi kabisa. Hakuna nia ya kusema watu waje na mabango ya kumtukana Rais, alimaanisha kama wana grievancies na yeye kama RC , basi hata mabango ya matusi waje nayo tu!
 
Kwa lugha rahisi unataka Makongoro aishi kama yuko Jela.

Maisha hayawezi kusimama kwakuwa eti mtu siyo mkuu wa mkoa.

Acheni kuabudu TEUZI.

Makongoro siku zote yuko hivyo, leo ana miaka karibu 60 ndio unategemea kwasababu umemteua Mkuu wa mkoa ndio atabadilika.
Unampotosha, kama hataki uteuzi ana uhuru wa kukataa.
 
Brother Mako

Najua wewe ni mtu wa masihara na utani utani mwiiingi. Utani hoye!

Najua wewe ndivyo ulivyo toka long time kitambo.

Ila nataka nikueleze kitu, Kuwa makini sana na utani wako usifikie hatua ya kuharibu haiba na taswira ya taasisi ya Urais au rais mwenyewe!. Namaanisha ukimtaja rais mtaje si katika muktadha wa masihara masihara, bali mtaje ukiwa serious na kwa vitu serious. Kama unataka kumtania rais basi acha hiyo kazi aliyokuteua, njoo JF tumtanie na tumchane kwelikweli akizingua!

Chalamila leo katumbuliwa, naamini sababu kubwa haswa ni ile clip aliyosikika akisema kuwa kwenye ziara ya rais huko Mwanza watu wanaweza kubeba mabango yoyote yale hata kama ni matusi! Naamini kabisa from the bottom of my heart kuwa Chalamila hakumaanisha kuwa watu wanaweza kubeba mabango ya Kumtukana rais, Bali alimaanisha kuwa watu kama wanahisi wana hasira dhidi ya utendaji wa mkoa wa Mwanza basi hata kubeba mabango ya kuwatukana viongozi wa mkoa huo mbele ya rais basi sawa tu!

Ukizingatia kuwa clip ya Chalamila imekatwa, watu wanaweza kushindwa kujua nini logic ya kauli yake. Hata hivyo Chalamila naye ameshindwa kutumia busara kwa kushindwa kujua kuwa kauli yake inaweza kutafsirika vibaya kuwa

1. Anacheza shere agizo la rais la kuruhusu watu kubeba mabango kwenye ziara zake.

2. Kwamba anamchukulia poa rais kwa kutoa kauli za mizahamizaha

Sasa ndugu Mako, kuwa Makini na mizahamizaha hasa juu ya maagizo ya rais. Mzaha ni bora uende vizuri ila ukienda vibaya, na wabaya wako wakaikatakata clip yako ili kukuchongea, hutaeleweka vizuri.

Nakushauri ndugu Mako, Fanya Mzaha 1% ila piga kazi 99%. Na mzaha wako usiinvolve jina la rais kabisa kwa sababu ukikosea pale utapata tabu sana.

Kumbuka busara za bungeni kwa nini kuna kanuni ya kutolitumia jina la rais kwa njia za mizaha ili kujipatia uhalali wa hoja.
Huyu chapii asipojirekebisha hamalizi mwaka atazinguliwa,ana mizaha ya kibwege bwege sana
 
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
Samia kateuliwa na magufuli? Alimteua akiwa kama nan
 
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
Yale ya mwigulu kumbe hayana ukweli!
 
Makongoro tena awe makini sanaaaa, mzaha mzaha hutumbua usaha, sasa Makongoro aache kabisa ule utani utani wake usio na maana, kazi kucheka cheka kila dakika moja kucheka cheka, aachane na hilo haraka sana, najua Makongoro sio mtu wa maendeleo kivile, na hilo ageuke haraka, awe mtu wa maendeleo haraka kwa watu wa Mkoa wa Manyara, aache story na kusema sema mambo ya historia, achape au aongoze watu wachape kazi.
 
"Kikofia hoyeee!!!,kifimbo hoyeee!!!......."

"Naenda shule yupoo!!![emoji1]...naensa jeshini yupo!!![emoji1]... naoa yupo!!!![emoji1] Hadi Leo nazeeka yupoooo!![emoji1]...."

Huyu mzee comedy Sana ana mixing Fulani ya mzee mchonga[emoji1]
 
Huyu jamaa labda humfahamu vizuri, Hakuna anachopoteza hata akitumbuliwa

Yeye ilimradi apate muda wa kukaa na washkaji jioni any we kahawa au chai au bia zake mbili baaas

Uteuzi sio maisha yake wala kutenguliwa hakutampa stress nakuambia

Maisha yake ni ya kijamaa sana na Itikadi ya kijamaa ikimuingia ndani ya damu yake

Usifikiri kuna watu wanateseka sana na hizi teuzi.

Ninamfahamu tangu zamani, angekuwa wa kung'ang'ania madaraka angefanya hivyo tangu zamani tu
 
Kwa lugha rahisi unataka Makongoro aishi kama yuko Jela.

Maisha hayawezi kusimama kwakuwa eti mtu siyo mkuu wa mkoa.

Acheni kuabudu TEUZI.

Makongoro siku zote yuko hivyo, leo ana miaka karibu 60 ndio unategemea kwasababu umemteua Mkuu wa mkoa ndio atabadilika.
Ndio namwambia mtoa mada kuwa CHEO hakimtishi wala kumbadilisha Makongoro

Aliishi hivyo kwa miaka kadhaa na kumtengua hakumpi stress
 
Ingekuwa mizaha inaathiri utendaji wa kazi na mwenye mizaha anatakiwa atumbuliwe mtu wa kwanza kutumbuliwa angekuwa Magufuli.
 
Huyu jamaa labda humfahamu vizuri, Hakuna anachopoteza hata akitumbuliwa

Yeye ilimradi apate muda wa kukaa na washkaji jioni any we kahawa au chai au bia zake mbili baaas

Uteuzi sio maisha yake wala kutenguliwa hakutampa stress nakuambia

Maisha yake ni ya kijamaa sana na Itikadi ya kijamaa ikimuingia ndani ya damu yake

Usifikiri kuna watu wanateseka sana na hizi teuzi.

Ninamfahamu tangu zamani, angekuwa wa kung'ang'ania madaraka angefanya hivyo tangu zamani tu
Siyo kila anayeteuliwa ana shida ya uteuzi. Ila heshima ya kuaminiwana na rais wa nchi ni kitu kikubwa, kuipoteza hiyo eti kusa una vijisenti viwili vitatu vya kunywa kahawa na bia na washikaji zako si jambo la kujivunia.
 
Kwa lugha rahisi unataka Makongoro aishi kama yuko Jela.

Maisha hayawezi kusimama kwakuwa eti mtu siyo mkuu wa mkoa.

Acheni kuabudu TEUZI.

Makongoro siku zote yuko hivyo, leo ana miaka karibu 60 ndio unategemea kwasababu umemteua Mkuu wa mkoa ndio atabadilika.
Watu ni wapumbavu sana yani wanataka watu wanyenyekee vyeo utafikiri vitawapeleka mbinguni.
 
Back
Top Bottom