Makontena ya Makonda: TRA wanatuhujumu au BANDARI wametuhujumu

Makontena ya Makonda: TRA wanatuhujumu au BANDARI wametuhujumu

Anaandika DOTTO BULENDO.....

Hapa ndipo "strong media" na "active citizens" wanatakiwa.

Kwanza tuliambiwa,wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi watachangia kutatua kero za elimu Dar es Salaam,makontena ya vifaa vya ofisini na vitabu yatakuja kutoka ughaibuni.

Baadae tukaambiwa si hayo tu bali na mengine yatatoka China kwa ajili ya maziwa ya watoto waliotelekezwa na mengine yataleta vitabu kwa ajili ya maktaba.

Baada ya hapo tukaambiwa Makontena yamefika yapo 36 yanavifaa vya maofinini kwa ajili ya ofisi za walimu kwa Shule za Dar es Salaam.

Baadae tukaambiwa hayatoki mpaka yalipiwe kodi kwani yamekuja kwa anuani ya mtu binafsi.

Baade tukaambiwa,kama TRA watataka yalipiwe kodi,wao na waziri wa fedha watashtakiwa kwa Rais.

Baadae tukaambiwa yanapigwa mnada ila yakapungua mpaka 20.

Baadae tukaambiwa atakaeyanunua atalaaniwa.

Baadae tukaambiwa,lazima yalipiwe kodi na aliyeyaleta na kama hatalipa yatapigwa mnada.

Baadae tukasikia waziri akisema,kama sheria ya kodi itapindishwa katika hili atakuwa tayari kumuomba Rais aachie ngazi.

Baadae tukamsikia Rais akisema,makontena hayo kwanza yana masofa na lazima yalipiwe kodi.

Baadae tukaambiwa mnada utapigwa leo jumamosi,

Baadae tunaambiwa mnunuzi kakosekana

Na sasa tunaambiwa kuwa kwanza hayo makontena hayana masofa kama tulivyoambiwa na vitu ni vichache sana eti vikipangwa vizuri yatabaki makontena yasiyozidi nane.

Haya mambo hayaaaaaa
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.Ila kaeni mkijua Tanesco wameshindwa kesi ya Standard Chartered na wanatakiwa kulipa mabilioni ya shilingi.

Chaguzi ndogo nazo zinaendelea,na pia jueni kuna kundi kubwa la vijana lililomaliza vyuo vikuu,vyuo na kwenye taasisi za elimu ya juu wanasubiri ajira tangu mwaka 2015.

Watumishi wa umma nao wanasikilizia kupandishwa madaraja pamoja na nyongeza ya mshahara tangu 2015.

Huku mfumo wa kodi ya mabenki ukitajwa kutikisa biashara na ustawi wa sekta binafsi.

Utekelezaji wa mradi wa Stigglers Gorge umeshaanza naona wanaharakati wanakimbilia vyombo vya magharibi kupiga kelele.

Simenti na yenyewe bado imegoma kushuka kama sukari.

Lakini jambo zuri ni sasa tunashuhudia kuanzwa kutandikwa kwa reli ya kati kwa kiwango cha Kisasa(SGR).

Haya mambo hayaaaaaa.Wasalaaam.

NB.Mwanasiasa akikuambia usiku mwema,usimuamini toka nje ukahakikishe kama
kweli usiku umeingia.

Sent using Jamii Forums mobile app
HATARI SANA!!!!!!!!!!!
 
Mi naona TRA hawakufanya makosa kukadiria kodi, mana mi kwa uelewa wangu TRA wanakadiria kodi kutokana na thamani ya mzigo iliyopo kwenye document ulizoagiziwa mzigo sio idadi ya kontena.
Kama ulivyo sema mtoa hoja inawezekana Mamlaka ya Bandari imefanya hujuma kwa kufungua makontena na kupunguza mzigo.
Pia haingii akilini kwamba mtu usafirishe mzigo unaotosha kontena kumi kwenye makontena ishirini afu unatoka sehemu moja, mana lazima gharama ya usafirisha iongezeke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nionavyo mimi
1.Kuna uwezekano mkubwa TRA wamekurupuka na kukadiria kodi isiyoendana na thamani halisi ya mzigo uliopo kwenye makontena,huenda hawakujiridhisha kilichomo ndani.
AU
2.Waziri wa fedha kakurupuka na kulibeba swala hili kichwa kichwa bila kujipa muda wa kutathmini mzigo ule na kiasi cha fedha kilichotajwa kama kilivyo naye bila ajizi akamjaza rais,huku umma nao ukapata cha kujadili bila kufikiri kama ilivyo kawaida yetu.
AU
3.Rais kaungizwa kingi,na tunajua kabisa mzee wetu huwa mtu wa "vuuup" bila kutafakari,hapa yawezekana kabisa kuna maslahi ya watu kumchonganisha DAB na baba yake kwa maslahi ambayo mimi na wewe tunayajua.
AU.
4.Waliopanga yale makontena huko ughaibuni hawana ujuzi wa kupanga mzigo kama tunavyo ambiwa ule ni msaada so hawakuzingatia upangaji kwa maana mzigo ule sio biashara so less care.
AU
5.Kuna uwezekano wa kuchezwa picha na mastermind wa ukweli kwamba mzigo umepakuliwa usiku ili kuua soo,na ndio maana mali inakosa wanunuzi,michezo ya Bandarini tunaijua vizuri sana...ila wanaopaswa kutupa ushuhuda wa kilichokuwa ndani ni wale waliofungua mzigo siku ya kwanza,otherwise mimi na wewe tukae kimya mana hatuji kabisa mwanzo na sasa kilichomo kwenye kontena ndicho chenyewe? tuache kushadadia.

MWISHO: Naona kuna watu wanaumbuka katika sakata hili na mwisho wa siku Mpakwa mafuta anaenda kuibuka mshindi maana taswira halisi inaonyesha hivyo...kitakachotokea ni hivi itafanyika tathmini halisi ya kodi mwisho wa siku watasema kodi ilikosema na kushushwa hadi milioni 100,200 au 300 which Daudi ataweza kulipa kwa mgongo wa kuchangiwa na washikadau wa DAR na mzigo kupelekwa mashuleni kama ilivyokusudiwa na Hadithi itaishia hapo huku maisha yakiendelea.
TRA hawakadirii tu kodi ila wanaangalia thamani ya mzigo wako kwenye document zako za mzigo, uwezi kua na document za mzigo afu hizo document hazioneshi thamani ya mzigo kua umeununua kwa sh ngp.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa sasa ule mzigo una thamani gani ?? kwa kila contena ni million kumi au million 70!!?? yaan tuchukulie kodi ni sawa na thaman ya mzigo
Kwa mujibu wa Troll JF , hapo maana yake thamani ya mzigo itakuwa hiyo kodi inayodaiwa na serikali jumlisha na gharama ya kununulia huo mzigo huko utokako kwa hesabu alizotoa maana yake gharama ya kununulia itakuwa kubwa kidogo kwa asilimia 20 zaidi ya bei ya kodi (hivyo bei ya manunuzi kujumlisha na kodi unapata thamani ya mzigo though watu wa bandari wao watauza kuhakikisha wanapata kodi yao na dalali anarudisha gharama zake)...naona mdau zachaja amedadavua kwenye comment yake #40
 
Kama unalipenda taifa hili na vizazi vyake, na kama unajua na kuamini kuwa kweli Mwenyezi Mungu yuko. Na ukitafakari mambo yaliyo kuwa ya naendelea katika taifa hili huko nyuma na dalili zinazo jichomoza sasa, basi elewa kuwa Taifa hili lahitaji kubadilishwa kiroho zaidi kuliko kimwili. Wote wanaotakia taifa hili mambo mema hawana budi kuchukua hatua za kiroho zaidi.

Mungu ana majira na nyakati zake, tuko tunaosubiri kwa saburi. Majira na nyakati za Bwana zifike, hakika zitafika tu.
 
Mi naona TRA hawakufanya makosa kukadiria kodi, mana mi kwa uelewa wangu TRA wanakadiria kodi kutokana na thamani ya mzigo iliyopo kwenye document ulizoagiziwa mzigo sio idadi ya kontena.
Kama ulivyo sema mtoa hoja inawezekana Mamlaka ya Bandari imefanya hujuma kwa kufungua makontena na kupunguza mzigo.
Pia haingii akilini kwamba mtu usafirishe mzigo unaotosha kontena kumi kwenye makontena ishirini afu unatoka sehemu moja, mana lazima gharama ya usafirisha iongezeke

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia kuna uwezekano mtu aliamini kabisa atasamehewa kodi hivyo akafanya package ya namna ile ili mwisho wa siku na zile container alikuwa na shida nazo kwa shughuli zingine baada ya kupakuwa mzigo hasa ukizingatia hata gharama ya kusafirisha watu wengine wamelipia. (mie mgeni kwenye haya mambo hizi container zikija na mzigo huwa zinaachwa bandarini au mzigo unabebwa na container lake na inakuwa mali ya mwenye mzigo)
 
mtizamo wangu binafs na kwa kupitia maoni ya watu waliofika mnadani, ule mzigo umepakuliwa na mzigo mwingi umeondolewa kwenye kontena!! nani atakua ameupunguza kwa siri?? hakuna mwingine bali mkubwa wa kazi Makonda. nguvu alizonazo hashindwi kufanya mchezo mchafu. pitieni sehemu mbali mbali zenye video toka bandarini mtakubaliana na mimi ule mzigo umepakuliwa na mwingi wametoweka nao.
Acha kuzungumzia hisia na na mawazo ya watu halafu unaleta kwenye kadamnasi tukuamini
Lete ushahidi kamili,kama huna bora ukae kimya badala ya kuendeleza uvumi unaopotosha watu
Wenyewe wanatuambia samani toka nje zinakadiriwa kwa kodi ya juu ili kupunguza uingizaji,pia samani hizo ni used kuna surchage ya uchakavu
Mbona hushangia mtu analeta gari mtumba mpaka linafika bandarini ni milioni tano ,anaambiwa alipe kodi milioni kumi
 
Hakuna container inayosafirishwa loose vile
Furniture zenye uwezo wa kuunganisha huwa zinawekaa kwa box
Wameshapakua vingine vyote visivyohusiana na shule bila shaka na kuacha vile tu vya kugereshea kuwa ni vya shule
 
Na
kila nikitizama picha na kuunganisha dot juu ya mnada wa makontena ya makonda na hatima yake naona kuna kamchezo pale!! mnada unashindikana kwa mara ya pili kwanini unashindikana??

sababu kubwa ni watu kutofika bei elekezi kutoka TRA. kwanini hawafiki bei? jibu ni moja mzigo hauna thaman wanayoitaka wao. sasa kwann mzigo usiwe na thaman hiyo wakati ilikadiliwa kodi tu ni 1.4 billion ina maana mzigo una thaman zaidi ya hiyo. lakn kwa haraka haraka mnada kwa makontena yote bei wanayofika haizid million 300. yaani millioni miatatu tuu!!.

sasa hapa kuna vitu vya kuhoji.

kwanini mzigo unaonekana hauna thamani inayotamkwa na TRA? ina maana chombo chetu hakina wataalam wa kukadilia thaman ya mizigo kiasi hiki?? lakn tofauti ni kubwa sana maana kwa kawaida kodi huwa haizidi thaman ya mzigo. sasa kwanini iko hivi??

pili mwenye mzigo hakulalamika kwamba makadilio ya kodi ni makubwa ina maana alilidhika nayo ile gharama, ila tu alitaka msamaha. sasa kwann mzigo uwe na thaman ndogo kiasi hiki??

mtizamo wangu binafs na kwa kupitia maoni ya watu waliofika mnadani, ule mzigo umepakuliwa na mzigo mwingi umeondolewa kwenye kontena!! nani atakua ameupunguza kwa siri?? hakuna mwingine bali mkubwa wa kazi Makonda. nguvu alizonazo hashindwi kufanya mchezo mchafu. pitieni sehemu mbali mbali zenye video toka bandarini mtakubaliana na mimi ule mzigo umepakuliwa na mwingi wametoweka nao.

huwezi kutoka na kontena USA ukapanga mzigo vile. et meza toka USA zimepakiwa zimefungwa tayari. pamoja na mizigo kuwa imeumganishwa tayari kwa matumizi harafu kamzigo kako nusu kontena huku makontena mengine yako robo. hakuna upangaji wa mizigo kama huo duniani kwenye biashara ya usafirishaji. ni hasara na ni hatari maana vitu vikipangwa vile ni rahis kuharibika. chunguzeni mtagundua yale makontena yamepakiwa hapa hapa bongo kwa kutupiwa tu mizigo kiduuchu danganya toto!! yale makontena 20 ukiyapanga kwa ustadi yatatoka makontena manne tuu!!!!

sasa hapa kuna hatari taasisi zetu kuchafuka kwa scandle mbili . moja BANDARI wameshilikiana na wahujumu mapato kupakua mzigo au TRA hawajui kazi wanabambikia wateja bei isiyo halali. zote mbili ni kashifa!!! kazi kwenu kijinasua TRA AU BANDARI.
Pia Polisi bandari walikuwa wapi hadi mchezo ukafanyika?
Bill of Lading inasemaje khs mzigo?
 
Mkuu ukiona Manyoya jua kesha liwa ,Wakubwa wamesha chota chao mapema na tukaachwa sisi kupiga Zogo tu.
 
Back
Top Bottom