Makontena ya Makonda: TRA wanatuhujumu au BANDARI wametuhujumu

HATARI SANA!!!!!!!!!!!
 
Mi naona TRA hawakufanya makosa kukadiria kodi, mana mi kwa uelewa wangu TRA wanakadiria kodi kutokana na thamani ya mzigo iliyopo kwenye document ulizoagiziwa mzigo sio idadi ya kontena.
Kama ulivyo sema mtoa hoja inawezekana Mamlaka ya Bandari imefanya hujuma kwa kufungua makontena na kupunguza mzigo.
Pia haingii akilini kwamba mtu usafirishe mzigo unaotosha kontena kumi kwenye makontena ishirini afu unatoka sehemu moja, mana lazima gharama ya usafirisha iongezeke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TRA hawakadirii tu kodi ila wanaangalia thamani ya mzigo wako kwenye document zako za mzigo, uwezi kua na document za mzigo afu hizo document hazioneshi thamani ya mzigo kua umeununua kwa sh ngp.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawa sasa ule mzigo una thamani gani ?? kwa kila contena ni million kumi au million 70!!?? yaan tuchukulie kodi ni sawa na thaman ya mzigo
Kwa mujibu wa Troll JF , hapo maana yake thamani ya mzigo itakuwa hiyo kodi inayodaiwa na serikali jumlisha na gharama ya kununulia huo mzigo huko utokako kwa hesabu alizotoa maana yake gharama ya kununulia itakuwa kubwa kidogo kwa asilimia 20 zaidi ya bei ya kodi (hivyo bei ya manunuzi kujumlisha na kodi unapata thamani ya mzigo though watu wa bandari wao watauza kuhakikisha wanapata kodi yao na dalali anarudisha gharama zake)...naona mdau zachaja amedadavua kwenye comment yake #40
 
Kama unalipenda taifa hili na vizazi vyake, na kama unajua na kuamini kuwa kweli Mwenyezi Mungu yuko. Na ukitafakari mambo yaliyo kuwa ya naendelea katika taifa hili huko nyuma na dalili zinazo jichomoza sasa, basi elewa kuwa Taifa hili lahitaji kubadilishwa kiroho zaidi kuliko kimwili. Wote wanaotakia taifa hili mambo mema hawana budi kuchukua hatua za kiroho zaidi.

Mungu ana majira na nyakati zake, tuko tunaosubiri kwa saburi. Majira na nyakati za Bwana zifike, hakika zitafika tu.
 
Pia kuna uwezekano mtu aliamini kabisa atasamehewa kodi hivyo akafanya package ya namna ile ili mwisho wa siku na zile container alikuwa na shida nazo kwa shughuli zingine baada ya kupakuwa mzigo hasa ukizingatia hata gharama ya kusafirisha watu wengine wamelipia. (mie mgeni kwenye haya mambo hizi container zikija na mzigo huwa zinaachwa bandarini au mzigo unabebwa na container lake na inakuwa mali ya mwenye mzigo)
 
Acha kuzungumzia hisia na na mawazo ya watu halafu unaleta kwenye kadamnasi tukuamini
Lete ushahidi kamili,kama huna bora ukae kimya badala ya kuendeleza uvumi unaopotosha watu
Wenyewe wanatuambia samani toka nje zinakadiriwa kwa kodi ya juu ili kupunguza uingizaji,pia samani hizo ni used kuna surchage ya uchakavu
Mbona hushangia mtu analeta gari mtumba mpaka linafika bandarini ni milioni tano ,anaambiwa alipe kodi milioni kumi
 
Hakuna container inayosafirishwa loose vile
Furniture zenye uwezo wa kuunganisha huwa zinawekaa kwa box
Wameshapakua vingine vyote visivyohusiana na shule bila shaka na kuacha vile tu vya kugereshea kuwa ni vya shule
 
Na
Pia Polisi bandari walikuwa wapi hadi mchezo ukafanyika?
Bill of Lading inasemaje khs mzigo?
 
Mkuu ukiona Manyoya jua kesha liwa ,Wakubwa wamesha chota chao mapema na tukaachwa sisi kupiga Zogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…