Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

Lugha, kama ilivyo kwenye mambo mengine, hubadilika na kukua.

Misamiati [msamiati] huongezeka, maana za maneno huongezeka na kubadilika, na kadhalika.

Mfano, kwenye Kiingereza sasa hivi neno ‘selfie’ ni neno rasmi kabisa lililopo kwenye kamusi za Kiingereza zinazotambulika.

Papo hapo, neno ‘groupie’ nalo lipo mbioni kuanza kutambulika rasmi kama uwingi wa neno ‘selfie’.

Kwa muda mrefu sasa neno ‘groupie’ limekiwa likimaanisha kitu kingine kabisa.

Lakini sasa limeongezeka maana.

Ni mambo ya kawaida kwenye lugha.
 
Nakuunga mkono. Ni makusudi siyo bahati mbays mfano mtu anaandika xaxa badala ta sasa, tubadilike
 
Tunaanza na maelezo yako. Huwezi kuwa na sentensi ndefu kiasi kama aya. Sentensi yako ya kwanza haieleweki. Baada ya orodha ya maneno uliyotoa, pia sentensi hiyo haileweki. Na umemalizia kwa kuweka alama ya kuuliza wakati mpangilio wa maneno yako haujafuata jinsi ya kuandika sentensi ya kuuliza.
Toa boriti kwanza ndio utoe kibanzi kwa mwenzio
 

Shida inaanzia shuleni za MSINGI ambapo malimu wengi makanjanja so watu wengi wanatoka huko wakiwa hawana uwezo wa kutofautisha sehemu zinazotakiwa kuwekwa H au kutowekwa pia na kushindwa kufahamu wapi pa kuweka L na R
 
Nadhani changamoto ni shule tulizosoma na ubora wa elimu ya kiswahili unaotolewa sasa ivi. Kiswahili cha kuandika kimepungua sana kiwango.
 
Matumizi ya neno onesha na onyesha ...inanikera sana hadi wasomi wa kiswahili wanakosea hapa
 
Skitt's Law: "Any post correcting an error in another post will contain at least one error itself."
 
Inakera sana mkuu
 
Mada muhimu kama hizi huwaoni hao watu maarufu wa humu jamvini.

Inasikitisha uzi wa Agosti na bado ni kurasa 1, wakati huohuo kinachojadiliwa kinaamsha tafakari jadidi.
Uko sahihi mkuu,mada fikirishi kama hizi hazizingatiwi sana
 
Mombasa na Lamu wanaongea kiswahili kizuri na fasaha kuliko sehemu yeyote ile Tanzania. Utashangaa sana ukiwasikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…