Umenikumbusha kitu nimekuwa nikijiuliza siku nyingi kichwani.
Kama neno MAONYESHO siku hizi limegeuka na kuwa MAONESHO; Je KUJA nayo inatakiwa iwe KUKUJA na KULA iwe KUKULA, pamoja na maneno mengie yanayofanana na haya?
Je, kwenye KIswahili hatuna IRREGULAR VERBS kama ilivyo kwenye Kiingereza? Kama hatuna, hayo maneo mawili nimetolea mfano hapa, yanaitwaje kwenye Kiswahili, sababu hayafuati utaratibu wa vitenzi vingine kama ilivyo kawaida kwenye Kiswahili?
Mfano mwingine
kitenzi kuta: mfano maneno siku-kukuta, nime-kukuta. Kinaanza na ku- kama ilivyo kwa mifano miwili hapo juu, lakini unaweza kuona mkanganyiko ulioko katika maneo haya mawili. Hili pamoja na kwamba limeanza na ku- lakini bado linaongezwa ku nyingine tena, tofauti na yale maneno mawili ya mwanzo niliyoyatolea mfano hapo juu
watafiti wa Kiswahili mpo hapa?