Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

kimsingi watu wengi hufanya makosa katika utumiaji sahihi wa lugha pasina kufahamu au kwa makusudi tu,na hii inatokana na factor mbali mbali ambazo mzungumzaji mwenyewe anazifahamu.
 
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema

Asante!

Umenikumbusha kitu nimekuwa nikijiuliza siku nyingi kichwani.
Kama neno MAONYESHO siku hizi limegeuka na kuwa MAONESHO; Je KUJA nayo inatakiwa iwe KUKUJA na KULA iwe KUKULA, pamoja na maneno mengie yanayofanana na haya?
Je, kwenye KIswahili hatuna IRREGULAR VERBS kama ilivyo kwenye Kiingereza? Kama hatuna, hayo maneo mawili nimetolea mfano hapa, yanaitwaje kwenye Kiswahili, sababu hayafuati utaratibu wa vitenzi vingine kama ilivyo kawaida kwenye Kiswahili?

Mfano mwingine

kitenzi kuta: mfano maneno siku-kukuta, nime-kukuta. Kinaanza na ku- kama ilivyo kwa mifano miwili hapo juu, lakini unaweza kuona mkanganyiko ulioko katika maneo haya mawili. Hili pamoja na kwamba limeanza na ku- lakini bado linaongezwa ku nyingine tena, tofauti na yale maneno mawili ya mwanzo niliyoyatolea mfano hapo juu
watafiti wa Kiswahili mpo hapa?
 
Kweli kabisa Mzee kifimbocheza.

Hayo pia yanaiharibu lugha yetu.
Pia kuna vijimaneno vya wanawake lakini cha ajabu waweza kukuta mtoto wa kiume anayatumia.
Hapo mi ndo kichwa huwa kinaniwaka, dume zima utakuta limeandika vineno vya kike
 
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema

Asante!
Kabila la kiha limechangia sana kuharibu kiswahili
 
Kila lugha INA pande mbili.. Lugha rasmi na ile ya mitaa(slang)..

Hakuna jamii ina lugha ambayo haina 'slang'..

Mbaya ni kuweka hayo maneno katika mazingira ambayo ni rasmi kwa mfano kwenye ofisi au machapisho mengine ambayo ni rasmi...

Slang inasaidia kufikisha ujumbe bila matumizi ya nguvu nyingi..

Ubaya mwingine ni kama mtumiaji wa slang anaitumia bila kulijua neno halisi
 
Ni kweli
Hivi uhandishi unamaanisha ndiyo nini ?
Kuna kukosea na makosa ya kawaida kwenye lugha! Kwa mtumiaji wa kila siku wa Kiswahili anafahamu "uandishi" linatokana na neno "andika" na ukiona mtu ameandika kinyume chake, basi amekosea!

Napata shaka kama uhandishi ni moja ya maneno ambayo yanakosewa sana kwenye Kiswahili! Kwa maana hiyo, naamini ulifahamu kabisa nilikuwa nalenga kuandika nini na kwahiyo, ulitakiwa kusahihisha kama alivyofanya mwenzako hapo juu! Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana utaona hata kwenye tungo husika, nilianza kwa kuandika "uandishi" lakini baadae nikaandika "uhandishi"
 
Naamini 'ga' mwishoni mwa kitenzi yamaanisha kitendekacho mara kwa mara.
Kwenye kiswahili hakuna maneno yanayoishia na ga ili kuonyesha hali ya kutendeka mara kwa mara. Maneno ya nakwendaga, namwonaga, naimbaga huwa sio sahihi. Japo moja ya sifa ya lugha ni kukuwa kwa misamiati lakini hayo maneno bado hayajafanyiwa utafiti na kuingizwa ili yatumike rasmi, vinginevyo yawekwe kwenye rahaja tu
 
Naona hata waalimu wanaandika hivyo ubaoni, maana haiwezekani asilimia kubwa wanaandika hivyo
Twaweza fuatilieni mtupe %
 
Nahisi ilikua ni kutafuta urahisi katika utamkaji wa baadhi ya maneno ambapo matokeo yake ata ule utamkaji pia tukauleta kwenye uandishi.

mfano neno "zumuni" linatamkika kirahisi mdomoni zaidi ya neno "dhumuni"
neno "angu" ni jepesi kutamka kuliko neno "wangu"
 
Habari za asubuhi wana JF?

Kumekuwa na tatizo la kiuandishi kwa watu wengi kuanzia humu JF mpaka kwingineko kote kwenye mitandao ya kijamii mwanzo nilidhani ni kujisahau lakini sasa naona kama imezoeleka na kuonekana kama ni maneno ya kawaida kwenye kiswahili na watu wala hawastuki kuona kama ni makosa,yaani makosa yakirudiwa rudiwa mara nyingi huzoeleka na kuonekana ni usahihi

Naomba nitoe mifano michache ya hayo maneno hapa chini;
Nisamee badala ya Nisamehe
Eshima badala ya Heshima
Asubui badala ya Asubuhi
Mdogo angu badala ya Mdogo wangu
Kiac badala ya kiasi
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei
Utamsikia Mtangazaji anasema Nyimbo hii badala ya kusema wimbo huu

Yako maneno mengi sana yanayopotoshwa na wadau wengi humu ndani,ombi langu tu ndugu zangu tubadilike tuandike maneno kwa usahihi wake kwa sababu humu ndani panapitiwa na wanafunzi kuanzia Shule za Msingi,Sekondari na hata Vyuo wanajifunza nini juu ya tunayoyaandika humu?

Eti hapo ndio tunawadharau Wakenya hawajui Kiswahili hawajui kiswahili wakati sisi wenyewe ndio tunavuruga tu.

Ni hayo tu wadau muwe na Jumapili njema

Asante!


Pole mkuu, hata mimi Jumamosi iliyopita niliandika mada yenye kichwa cha habari "Mtihani wa Kiswahili kwa rais Magufuli". Unaweza kusoma kwa undani zaidi nilichoandika hapo chini.

Lugha yetu ya Kiswili ni moja kati ya lugha maaarufu hapa duniani na kwa sababu hii yapaswa tujivunie. Lakini si hivyo tu, yapaswa pia kuilinda na kuiendeleza ili izidi kuwa maaarufu. Kwa bahati mbaya nafikiri kama taifa tunapoteza mwelekeo wa kuienzi lugha yetu na mimi nikiwa kama mzalendo wa nchi yangu najisikia nina jukumu la kutoa mchango wangu.

Pamoja na tofauti za kifikra kwenye baadhi ya mambo kati yangu na rais Magufuli lakini kuna kitu kimoja kinatuunganisha, kupenda lugha yetu ya Kiswahili. Kwa sababu hii natuma ombi langu moja kwa moja kwa rais ili tuweze kuijenga lugha yetu na naamini kama akisoma ujumbe huu atachukua hatua. Wengine wanaweza kupuuza wito huu na kuona una umuhimu mdogo kwa taifa lakini si kweli kwa sababu nitakazo zielezea. Kwa mfano, moja ya sababu kwanini filamu, nyimbo na vitabu vya Kiingereza ni maarufu ni kwasababu lugha hiyo inaeleweka sehemu nyingi duniani. Ndio maana wasanii wao nao pia wanakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu wana soko kubwa ukizingatia kuwa kazi zao zinanunuliwa sehemu mbalimbali duniani na kuingizia mapato serikali zao kutokana na kodi. Sababu hiyo hiyo pia ndio inawafanya wasanii wetu wafanye vizuri hususani hapa Afrika Mashariki kutokana na watu kuielewa lugha ya Kiswahili. Mpaka hapa utaona ni kwa jinsi gani lugha inaweza kuinua wasanii na kuchangia pato la taifa.

Lakini pia kuna changamoto zinazoikabili lugha yetu na ili kuhakikisha inaendelea kuwa lugha ya kuvutia kuna hatua inabidi zichukuliwe. Kuna changamoto kubwa mbili nimeona nizitaje.



1. Kutojivunia lugha ya Kiswahili

Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kuongea lugha ya Kiswahili sanifu lakini cha kusikitisha kuna baadhi ya watu hawajivunii Kiswahili. Kwa mfanao kuna baadhi ya watu hawawezi kuongea sentensi moja bila kutia neno la Kiingereza. Kuna siku moja hapa Jamii Forums nilimkosoa bwana mmoja tena ni mwandishi wa habari kwa kuchanganya maneno ya Kiswahili na Kiingereza kwenye sentensi. Nilimwambia kama mimi ninakaa Ulaya kwa karibu miaka ishirini na nina mke na watoto ambao wanaongea Kiingereza nyumbani kwangu lakini bado naandika Kiswahili fasaha kwanini wewe usiweze? Akanijibu kwamba wakati mwingine ni rahisi kujielezea kwa lugha ya Kiingereza kitu ambacho sikubaliani nae kwa asilimia mia. Naelewa kuwa wakati mwingine unaweza kuazima maneno lakini kuna watu wanapenda kuazima maneno mengi ya Kiingereza bila ya ulazima. Ni kitu ambacho kinakera zaidi kuwaona watangazaji na watu maharufu wakitumia maneno ya Kiingereza pasipo na lazima na wao ndio kioo cha jamii.



2. Kukosekana kwa chombo madhubuti cha kuboresha Kiswahili

Aya hii ndiyo ningependa rais aingalie kwa makini zaidi kwakuwa inaihusu chombo kinachosimamiwa na serikali. BAKITA kama chombo cha kusimamia Kiswahili Tanzania sidhani kama kinafanya kazi nzuri. Kazi wanayoifanya nina uhakika hata ukimpa mtoto wa miaka saba pia ataweza kuifanya. Nafikiri BAKITA ina watu wavivu na wakosefu wa ubunifu. Yaani kila neno lazima lianze na ki…, kwa mfanao, kicharazio (keyboard), kitanza mbali (remote control) n.k. Nina uhakika hata ukiiambia BAKITA ibuni tafsiri ya rocket watakwambia kiendea mwezini, kazi ambayo hata mtoto wa miaka saba anaweza kuifanya. Au maneno mengine kama runinga (television), neno limekaa utafikiri la Kinyarwanda vile. Kwani mpaka kila neno liwe na kifanyia hivi, kifanyia vile... Lugha ni nzuri lakini kuna mijitu inataka kuiharibu kwa ajili ya uvivu wa kufikiri halafu inalipwa mshahara na pesa za walipa kodi.


Ningependekeza serikali iiangalie kwa karibu BAKITA na kuhakikisha inafanya kazi kwa ubunifu wa maneno mazuri ya Kiswahili. Pia kuchukua hatua ya kuwabadilisha wale wenye majukumu ya kubuni maneno mapya ya Kiswahili mara moja pale inapoonekana wanazembea.

Serikali kuwaadhibu waandishi wa habari na watangazaji ambao watashindwa kutumia Kiswahili sanifu. Kwa mfano, kuyapiga faini magazeti vya radio na runinga pale inapobainika wafanyakazi wao wanashindwa kuongea Kiswahili fasaha au wanapoazima maneno ya Kiingereza bila sababu ya msingi.

Huu ni mtihani wako rais Magufuli na naamini kwa sababu wewe ni mpenzi wa Kiswahili kama mimi hutaniangusha.
 
Mnaosema aachane na hii kampeni ya kukazania ukuzaji wa Kiswahili fasaha mtakuwa hamjafuatilia matokeo ya form 4 katika somo la Kiswahili. Wanafunzi wengi walifeli katika somo la Kiswahili. Chanzo chake ni hii mentality ya kuendelea kunyamazia ubovu huu. Kila kitu kilichoharibika kisipotanguliwa au kufanyiwa marekebisho matokeo yake ni Mabovu zaidi. Lingine nyie mnaoona si jambo la maana kuongea Kiswahili fasaha mtakuwa wa kwanza kumcheka Mtanzania mwenzenu pindi aongeapo Kiingereza kibovu. Wenzetu watumiaji wa lugha nyingine hutawaona wakiacha lugha zao ziharibike katika matumizi ya Television, Radio, au mitandaoni kama tufanyavyo. TUBADILIKE!!!
 
Mkuu Chige ninaomba msaada wako kuna jamaa yangu mfaransa anajifunza kiswahili. Huwa ananiuliza maswali ya kiufundi nyakati nyingine, ambayo kimsingi ni nje ya taaluma yangu.

Nimeona kwa uchangiaji wako, nikahisi waweza kuwa ni wa msaada. Nina c&p ujumbe chini wa swali husika la huyo mgeni:

Rafiki, I have a question

There is a sentence:
Wanawake niliowaona ni wazuri.
Is that correct?

Siwezi kufaham kwa nini kuna -wa- ndani ya "verb".
There is the relative -o- and I can get that (The women THAT I saw...), but why the repetition of "women" in -wa-?

Why should we repeat the relative -o- and the object -wa- (wanawake)?
Hahahaha! Mkuu wangu, binafsi sio mtalaamu kiasi hicho hususani linapokuja suala la uchambuzi wa sarufi, kwa sababu mimi ni mwandishi tu wa kawaida ambae msisitizo wangu ni kuhakikisha naandika tungo sahihi kisarufi. Kimsingi, sina uwezo wa kuichambua sarufi kiufundi namna hiyo.

Lakini nikirudi katika matumizi ya kawaida tu, hiyo sentensi sioni kama ina tatizo lolote. Na wala siioni kama ni miongoni mwa zile sentensi ambazo huwa tunafanya sana makosa! Kwa mfano:

Mimi binafsi napenda kutumia Kiswahili kuliko lugha nyingine yoyote ile.

Ukiangalia kwenye hiyo sentensi, utaona maneno mawili ya mwanzo, lolote moja wapo halikutakiwa kuwepo.
 
Badala ya kusema 'anakujaga' unapaswa kusema 'huwa anakuja'. Hiyo ndio huonesha kitendo cha mara kwa mara.
Naamini tatizo haswa ni uandishi unaofuatia matamshi potofu. Pale lafudhi inapopelekea 'L' na 'R' kutamkwa visivyo na hatimaye maandishi kufuata mkondo.
Ila bado maboresho katika lugha huzaa misamiati na hili la 'ga' kumaanisha tabia ya kitenzi ni mfano.
Kadhalika maneno kufupishwa na kuunganishwa kama 'hawa 'anakula' kuwa 'hula' ni kawaida. Na ukiongeza 'ga' yaeleza kasi ya tendo kurudiwa
 
Back
Top Bottom