Kuna maneno kwa kweli yanaudhi, sio tu kuyasikia bali hata kuyasoma!
Halafu kuna neno aghalabu! Neno hili watumiaji wengi wa Kiswahili hupindua tafsiri yake, kutoka mara nyingi na kudhani ni (huzani?) ni mara chache!! Aidha, mara nyingi matumizi ya neno "tegemea" huacha ukakasi mwingi nyuma yake.
Yote tisa, donda ndugu lipo kwenye "r" na "l". Inakera sana kuona mtu anatamka au kuandika "naludi saa tano manake mala kwa mala huo ndio muda wangu wa kuludi kazini!"
Tusisahau pia neno saa linapotamkwa au kuandikwa kwa wingi kwamba masaa! Hapa utakuta hata Waandishi wa Habari wakisema "Waziri Mkuu alihutubia kwa masaa matatu!
Nilisahau! Ingawaje maneno yapo mengi mno kiasi kwamba siwezi kuyataja japo robo yake lakini wacha tu nilizungumzie hili neno "aidha."
Watumiaji wengi wa Kiswahili wanalitumia neno "aidha" kama "either" la Kiingereza, wakati tafsiri ya neno "aidha" ni "vile vile", "pia" au neno lolote lenye tafsiri sawa na hayo. Hivyo basi, badala ya kusema mathalani, "natarajia kuhamishiwa aidha Morogoro au Dodoma", hapo ulitakiwa kusema "natarajia kuhamishiwa ama Morogoro au Dodoma!"
Lakini mleta mada, nawe unatakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya utenganishi wa maneno. Inaleta ukakasi kuona unaandika maneno zaidi ya thelathini na hakuna kituo pahala popote pale kwenye tungo husika.
Kwavile umehusisha matumizi mabaya ya Kiswahili na uandishi, basi pia tukumbushane uhandishi sahihi ni pamoja na matumizi sahihi ya utenganishi wa maneno; yaani punctuation.