Makosa makubwa; Nembo ya Taifa imebadilishwa kwenye mihutasari mipya ya masomo Shule ya Msingi

Makosa makubwa; Nembo ya Taifa imebadilishwa kwenye mihutasari mipya ya masomo Shule ya Msingi

Hivi ni kazi kubwa kiasi gani kwenda shuleni ukaangalia hiyo mihutasari? Sehemu za kupata soft copy za nyaraka za serikali kama hizo pia hamzijui?

Washambuliaji wengi wenu msije kuwa ndio waandaaji wenyewe wa ile mihutasari! Acheni kutafuta kujishikiza mahala pasipo shikizika jambo la msingi rekebisheni Nembo ile au kama ni sahihi kuwa vile basi toeni ufafanuzi tulioona tatizo tutokwe na utata wa jambo hilo.
Weka picha mkuu... Kuna wengine hawana muda wa kwenda huko shule lakini lakini tatizo hilo linaweza kushughulikiwa
 
Yaani hata mniite zwazwa, kiazi au jina baya gani bado sitaweza kuleta picha hapa kwa sababu mimi ni mtumishi na natambua maadili ya utumishi!
Nani anajua kua wewe ni mtumishi au siyo mtumishi?
Yawezekana Una skills ndogo ndomaana unasema huwezi kupandisha picha,yaani skills za matumizi ya device yako.
 
Bila ushahidi wa picha unatulazimisha tuamini tu maneno yako kisha tuendelee kujadili mada. Hiyo haiko sawa, taarifa yako haijakamilika.

BTW, huo muhtasari sio public document?? Hayo maadili gani unayoyazungumzia?
 
Walimu ni waoga sanaa.. Hasa kwenye mambo ya kweli..
Wahenga wanasema shoka bila mpini haliwezi kukata mti 🌳.
 
Hayo ni madhara ya designer wavivu wa kitabu, chapisho au waraka kwa kupakua picha mitandaoni.
Wazembe wengine ni editors na proof readers.
 
Wamerekebisha, mliochukua hatua hongereni na mliobeza poleni!
 
Trainee hongera sana kwa kupiga kelele kuhusu suala muhimu kwa taifa letu. Usichoke kusahihisha mambo kama kuna utata.
 
Back
Top Bottom