Makosa makubwa ya Muswada wa TISS


Wako kisiasa zaidi, na kazi yao kubwa ni kuhakikisha ule msemo maarufu wa Makada wa CCM kuwa CCM itatawala milele. Ukishaona usalama wa taifa wanapatikana kwa kujuana basi ujue hapo hakuna usalama wa taifa, bali usalama wa viongozi.

Walichokifanya uchaguzi wa SM 2019 na uchaguzi mkuu 2020, ule ulikuwa ni ushahidi kuwa usalama wa taifa wako kwa ajili ya maslahi ya CCM. Hivi sasa wanapewa nguvu hiyo kisheria, na hawataruhusiwa kushitakiwa! Machafuko ama serikali kupinduliwa, ndio yataondoa hizi sheria zenye nia ovu ndani ya nchi hii.
 
Kama huwa wanafanya yote haya unayosema...vipi kuhusu wizi uliowekwa wazi kwenye ripoti ya CAG walikuwa wapi?
Usiwe na haraka!, ripoti ya CAG ni ripoti ya ukaguzi, hivyo matumizi yoyote ya fedha za umma ambazo hazikufuata taratibu, CAG anaripoti, hivyo sio lazima iwe ni wizi!. Subiria Bunge la November.
P
 
Si lazima kila afisa wa TISS asijulikane, wanaweza kuwa na idara iliyo wazi kwa makosa maalum na maafisa wakafika mahakamani kutoa ushahidi.

Hata nchi zilizoendelea kuna issue za kipolisi, zingine FBI na pia CIA! Sheria ni nzuri ila inataka kuangaliwa kwa kina kuepusha kuingiliana majukumu.
 
Kuna tofauti kubwa. Kunusa kwa siri ni tofauti sana na kuwa na mamlaka kisheria ya kumkamata na kumpekua mtu.

Kwa mfano huyo afisa usalama ambaye sheria inataka utambulisho wake uwe siri akija kukukamata atajitambulisha?? Au atakuvamia tu kama jambazi na kukuteka?

Nini kitawazuia watu wenye nia ovu kujifanya ni ma 'afisa usalama' kisha wakawa wanateka na kuibia watu?

Utaratibu wa ukamataji watuhumiwa umewekwa sio tu kwa lengo la kulinda haki za mtuhumiwa, bali pia kuwalinda askari waonafanya ile kazi. Likija kundi la watu ambao hawajulikani kutaka kukuteka kama unao uwezo wa kujilinda unayo haki ya kuwamaliza kabisa kama alivyofanya Zakari. Lakini siku ile laiti wangeenda polisi wenye uniform bwana Zakaria asingethubutu kuwapiga risasi.
 
Kama wanaona jeshi la polisi halina ufanisi kwenye upelelezi na wanatamani kuwa na taasisi kama FBI basi ni afadhali waanzishe taasisi mpya ya kufanya kazi hizo pamoja na kulinda viongozi.
Ishu ni Ufanisi au kuuza taarifa wakati wa arrest au mwenendo wa uchunguzi?
 
Mkuu endelea kuwafunda ili wabadilike.
 
Naona unaamini kuwa watanzania wataendelea kuwa mazombie wa kudumu.
Tuna watu wa aina mbili, the wishful thinkers na the realists. Wishful thinkers ni wale wanao wish tuu!, hata the impossible, they'd wish. The realist ni wale wanadeal na the reality only. Mimi ni realist, hatuna Watanzania wa kuleta machafuko, wala Watanzania wa kupindua nchi!.
Keep on wishing!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…