Makosa makubwa ya Muswada wa TISS

Makosa makubwa ya Muswada wa TISS

Tuna watu wa aina mbili, the wishful thinkers na the realists. Wishful thinkers ni wale wanao wish tuu!, hata the impossible, they'd wish. The realist ni wale wanadeal na the reality only. Mimi ni realist, hatuna Watanzania wa kuleta machafuko, wala Watanzania wa kupindua nchi!.
Keep on wishing!.
P
Usichanganye reality na kujipendekeza bro.
 
MAKOSA MAKUBWA YA MSWADA WA TISS

Sehemu ya 1.

Moja ya makosa ya mswada wa sheria ya Usalama wa Taifa, kipengele cha 5 cha mswada huo kinampa mamlaka Afisa usalama kukamata na kupekua viongozi, hapa Kifungu hicho kina kinakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayosema kila mtu sawa mbele ya sheria, Kifungu kinaweka tabaka kwamba viongozi wa kitaifa hawatawajibika mbele ya sheria ya makosa ya jinai inayosimamiwa na jeshi la polisi, Viongozi wote watakuwa na sheria yao na chombo chao cha kuwakamata, kuwapekua na pengine wanaweza kuwa na mahakama zao.

Duniani kote Afisa usalama hafanyi kazi ambazo ni za wazi. Ukishamruhusu akamate na kupekuwa ni automatically umeamrisha afisa usalama huyo afike mbele ya mahakama kutoa ushahidi wa mtuhumiwa kama mkamataji na mpekuzi. Kazi hii iliwekwa kwa Idara ya upelelezi pekee na sio TISS.

Ajabu katika mswada huohuo, unajipinga katika kifungu cha 16 ambapo umeweka katazo la Afisa usalama kutotajwa wala kutojulikana popote yeye binafsi na kazi zake. Unajiuliza hivi hawa walipoweka kifungu cha Afisa usalama kukamata na kufanya upekuzi walijua hata onekana na kujulikana? Wanafahamu taratibu za ukamataji na upekuzi huanzia kwa Mwenyekiti/mjumbe wa mtaa/kitongoji na kisha mashahidi wa mtuhumiwa ndipo mtu apekuliwe? Je hapo afisa huyo atakuwa kafichwa utambulisho wake, sura yake au?

Mswada huu ni wa hovyo na haufai kabisa kupitishwa kuwa Sheria. Ukipitishwa kama ulivyo ni automatically hatutakuwa na Usalama wa Taifa, bali tutakuwa na Jeshi jipya lililochukua nafasi ya Idara ya Polisi ya upelelezi tu.

Dunia inapambana kufanya mageuzi Mashiriks ya Ujasusi yawe na mrengo wa kuhami uchumi, Lakini Serikali ya CCM imeleta mswada unaoirudisha TISS nyuma kuwa genge la kisiasa kulinda madaraka rasmi kutoka awali kuwa TISS ilifanya shughuli za kisiasa/kichama kinyemera, Sasa Rais Samia anairasmisha kuwa kikundi cha kulinda na kutetea madaraka ya kisiasa. Very sad!

Napendekeza kifungu hiki cha 5A kirekebishwe, TISS isihusike na ukamataji wala Upekuzi wa mtu yoyote katika nchi, isipokuwa ipewe idhini ya "kudhibiti" kwa mtindo wa elimination ama equity/excute katika eneo muhimu tu. Ukamataji na upekuzi ubakie kwa Idara ya upelelezi ambayo ndio itahusika na mambo ya Mahakamani pia. Kifungu cha 16 kirekebishwe, kimeweka mkazo sana katika kuficha utambulisho, dunia ya Teknolojia ni vigumu sana kwa maafisa kuficha utambulisho wake, badala yake kazi/Oparesheni ndio ziwekwe kwenye sheria ya kuzuia utambuzi wake.

Leo naomba niongelee juu ya contradiction ya vifungu hivi viwili cha 5A na 16 vya mswada huu, kati ya vifungu 27 vya marekebisho ya sheria ya Usalama wa taifa.

Na Yericko Nyerere
View attachment 2641730View attachment 2641731View attachment 2641733
Mbona wamewwka wazi kuwa wanataka hiyo idara iwe sawa na majeshi mengine!
Nchi inaelekea kwenye shimo la upumbavu kwa kasi sana
 
Si lazima kila afisa wa TISS asijulikane, wanaweza kuwa na idara iliyo wazi kwa makosa maalum na maafisa wakafika mahakamani kutoa ushahidi.

Hata nchi zilizoendelea kuna issue za kipolisi, zingine FBI na pia CIA! Sheria ni nzuri ila inataka kuangaliwa kwa kina kuepusha kuingiliana majukumu.
Maafisa Usalama wengi tu wanajulikana huku wilayani na mikoani.Kuna maafisa usalama wa mikoa kama vile Regional Security Officer (RSO) na wa wilaya District Security Officer (DSO). Hawa huwa wanajitambulisha hata kwenye mikutano ya hadhara.
 
Tuna watu wa aina mbili, the wishful thinkers na the realists. Wishful thinkers ni wale wanao wish tuu!, hata the impossible, they'd wish. The realist ni wale wanadeal na the reality only. Mimi ni realist, hatuna Watanzania wa kuleta machafuko, wala Watanzania wa kupindua nchi!.
Keep on wishing!.
P
Naunga mkono hoja.Nyerere aliijenga nchi hii vizuri sana.Ni nchi yenye umoja na mshikamano wa kutosha.Upinzani ungekuwa na nguvu ungeweza kuleta machafuko.Lakini sasa hivi ndiyo unadhoofika zaidi.

Na sababu ni CCM kujiendesha kama Kanisa Katoliki ambalo kila lilipokutana na upinzani wa watu kama akina Martin Luther baadaye lilijitafakari kubaini wapi linakosea.Halafu linafanya mageuzi.
CCM pia ikiona inakabiriwa na upinzani sana huwa inakaa na kujivua gamba kwa sababu upinzani hutokana na kujisahau CCM yenyewe kwa kutotekeleza sera za kuondoa kero za wananchi.
 
Mtu ukiwa ni realist, utasimama na ukweli daima, haijalishi ma wishful thinkers wanakuonaje. Nakiri the dividing line between kusifia kwa reality na kusifia kwa kujipendekeza is very thin!.
P

Reality ipi father unasimamia? Labda kama neno reality limepoteza maana yake siku hizi. Katika mazingira ambayo kusifia ni added advantage ya kutoka kimaisha, kujipendekeza hutafsiriwa kama kusimamia reality. Ili nisikivunje moyo, ngoja tufanye unasimamia ukweli.
 
Kiukweli naumia sana kila ninapo onekana kama chawa pale ninapo sifia for reality mtu anayestahili sifa. The only difference between pongezi za kweli na pongezi za kichawa ni very thin, machawa sio critical wao ni kufagilia tuu, mimi ni critical unayensifia leo tukamsifu, kesho akichemsha utamkosoa. Machawa are never critical.
P
 
Maafisa Usalama wengi tu wanajulikana huku wilayani na mikoani.Kuna maafisa usalama wa mikoa kama vile Regional Security Officer (RSO) na wa wilaya District Security Officer (DSO). Hawa huwa wanajitambulisha hata kwenye mikutano ya hadhara.
Mi namjua jamaa alijitambumisha kama RSO kwenye send off ya dada wa mke wangu[emoji1787]
 
Maafisa Usalama wengi tu wanajulikana huku wilayani na mikoani.Kuna maafisa usalama wa mikoa kama vile Regional Security Officer (RSO) na wa wilaya District Security Officer (DSO). Hawa huwa wanajitambulisha hata kwenye mikutano ya hadhara.
Hii ni matokeo ya good governance.. ila kabla ya hapo walikuwa hawatambuliki
 
Kiukweli naumia sana kila ninapo onekana kama chawa pale ninapo sifia for reality mtu anayestahili sifa. The only difference between pongezi za kweli na pongezi za kichawa ni very thin, machawa sio critical wao ni kufagilia tuu, mimi ni critical unayensifia leo tukamsifu, kesho akichemsha utamkosoa. Machawa are never critical.
P
Pascal si lazima wewe ujue kuwa ni chawa..pamoja na kujaribu sana kukuelimisha.
 
Ukiona Kuna kitu hukielewi vizuri jua hakikuhusu wapo wanaoelewa zaidi ya ulipoishia wewe(nawaza tu).
 
Kiukweli naumia sana kila ninapo onekana kama chawa pale ninapo sifia for reality mtu anayestahili sifa. The only difference between pongezi za kweli na pongezi za kichawa ni very thin, machawa sio critical wao ni kufagilia tuu, mimi ni critical unayensifia leo tukamsifu, kesho akichemsha utamkosoa. Machawa are never critical.
P
Ni ngum sana kwako kujisafisha ulishachafuka
 
Back
Top Bottom