Makosa Matano Makubwa Yanayokwamisha Malengo ya Vijana Wapambanaji

Makosa Matano Makubwa Yanayokwamisha Malengo ya Vijana Wapambanaji

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
3,240
Reaction score
5,625
Habari zenu wakuu
Nianze na kibwagizo cha wimbo wa mwanahiphop nguli Tanzania anayejulikana kama Dizasta Vina kwenye wimbo wake unaoitwa Get better aliyemshirikisha Beno Mwampamba

Mwampamba anaanza kwa kusema

"Leo imeshakuwa jioni
Na matokeo tuliyotegemea kuwa mbioni
Hata dalili zake hatuzioni
Hivi vitu vinavunja imani
Vinaleta simanzi
Ila sisi ni simba wenye njaa kali
Bila windo hatulali"

Nirudi kwenye mada kuu vijana wengi huwa tuna malengo mbalimbali ambayo tumepanga kuyatimiza kwa mda fulani lakini changamoto kubwa imekuwa ni jinsi ya kuyatimiza malengo hayo

Kumekuwa na makosa makubwa ambayo tunayafanya kama vijana ambapo kwa namna moja ama nyingine yanachangia kwenye mkwamo huu.

Yafuatayo ni mambo hayo

1. Kutokuweka Malengo Yenye Maana
Vijana wengi huishi kwa mtindo wa siku kwa siku, bila malengo wazi. Hakuna hatua thabiti ya kuchukua

2. Kutafuta Mafanikio ya Haraka
Wengi wanataka kufanikiwa haraka, bila kutambua kuwa mafanikio ya kudumu yanahitaji uvumilivu na juhudi.

3. Kutegemea Bahati Badala ya Kazi
Wengi hufikiri kuwa mafanikio yanatokana na bahati tu. Huu ni mkakati hatari.

4. Kukosa Msingi wa Kujitambua
Hapa ndipo siri kubwa inapoishi! Kujua wewe ni nani, ndilo litakalokufanya ushinde kila changamoto.

5. Kukataa Kujifunza Kutoka kwa Wengine
Vijana wengi wanajivunia kujua kila kitu, lakini wanakosa nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine.

Kufahamu makosa haya ni hatua muhimu kuelekea mafanikio. Kila changamoto ni fursa ya kujifunza na kuboresha, hivyo basi, jifunze, jiwekee malengo na endelea kupambana kwa kujitambua.

Credit to MpushyOfficial

Kwa wale wanaohitaji huduma ya kuprint uniforms,jezi,stickers,business cards,mabango n.k

Huduma ya picha mbao kwa ajili ya kumbukumbu,zawadi,urembo huduma ipo bora sana na kwa gharama nafuu ukiwa mahali popote Tanzania huduma itakufikia

Mawasiliano nicheck whatsapp 0615321080

Nimalizie na

John Calvin Maxwell aliyekuwa mwandishi wa vitabu mmarekani ana msemo wake maarufu unasema "Fail early and fail fast"

Mchana mwema
1753439226560.jpg
 
Kila kitu kinachukua Muda mrefu mfano MTU aliyesoma Shule za kata akasoma chuo Tanzania ili ajue angalau lugha ya kiingereza vizuri anabidi ajipe miaka 10 baada ya kutoka chuo
 
Siri kubwa ipo kwenye;
Nidhamu,
Uaminifu na
Kujiwekea malengo,

Kwenye uaminifu ndipo panapowarudisha nyuma vijana wengi,
Vijana wamekosa uaminifu kabisa,so inakua ngumu kuaminiwa,kingine ni uvivu na kutokujua thamani ya muda.
Mimi nawatetea vijana waajiriwa. Unakuta kijana anamiaka 27+ (graduate), anaajiriwa tu anakutana na mshahara wa laki 4. Pale kazini anafanya kazi za kupitisha Mamilioni.

Kijana huyo anaamua kuvumilia akiamini atapandishiwa maslahi. Inapita miaka kadhaa anaongezwa sh 50000/- kwenye mshahara na anapandishwa cheo. Hapo akifikiria kuanzisha familia, akifikiria kusaidia wazee wake, anaona kabisa hawezi kufika malengo bila kuwa mjanja mjanja (no risk, no story)

Private sector inavunja sana uaminifu wa vijana.
 
Back
Top Bottom