Makosa ndani ya Makala ya Mama Maria Nyerere Kutimiza Miaka 93

Andika kitabu tujifunze na tuone historia ya uhuru wa Tanganyika.
Naamini huwezi na hutaweza. Wameshindwa wenzio wengi walioahidi kufanya hivyo.

Wenzio waliokuwa wanampinga Mzee Mohamed Said na wameshindwa hoja,
huu uzi wanaupitia kimyakimya. Wenzio walipinga kwa hoja nzito lakini
mwisho walikimbia.

Kusimamia batili ni kazi ngumu sana.
 
Mama...
Nimeegemea kwa Sykes kwa sababu ndiyo walioasisi African Association 1929 kisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Naegemea kwao kwa kuwa ukimtoa Martin Kayamba ndiyo pekee walioandika historia ya nyakati zile kueleza mambo yalikuwaje.

Naegemea kwa Sykes kwa kuwa huwezi kuandika historia ya AA, TAA na TANU bila kusoma nyaraka zao.

Naegemea kwa Sykes kwa kuwa huwezi kumweleza Julius Nyerere katika harakati za TANU kama hujapita kwao.

Katika waasisi 17 walioasisi TANU wawili ni watoto wa Kleist Sykes muasisi wa AA.

Baba muasisi wa AA watoto waasisi wa TANU.

Ikiwa Uislam unakupa shida hilo litakuwa tatizo kubwa kwako kwa sababu Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika viongozi wake ni walewale waliokuwa wakiongoza AA - Kleist Sykes na Mzee bin Sudi na katika TANU wakawepo Ali Mwinyi Tambwe na Iddi Faiz Mafungo.

Mimi sina nguvu ya kulazimisha chochote.

Waliosoma kitabu changu ndiyo waliokifanya kitabu hiki kiwe juu na kutolewa matoleo manne.
 
Hatuwezi wote tukawa waandishi ila haitunyimi nafasi ya kukosoa mtu anapotaka kupotosha umma.
 
Hatuwezi wote tukawa waandishi ila haitunyimi nafasi ya kukosoa mtu anapotaka kupotosha umma.
Mama...
Lakini unakosoa nini?
Kuwa mimi babu yangu Salum Abdallah yote aliyofanya katika kuongoza migomo mitatu (General Strike) 1947, 1949 na 1960 si kweli ni uongo; kuwa ni muasisi wa TANU si kweli, alikuwa kiongozi wa TRAU 1955 si kweli unakosoa nini?

Kuwa African Association ilianzishwa na babu zangu si kweli.
Kuwa baba na babu zangu waliakuwamo katika TAA na TANU si kweli.

Kuwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilikuwa ndani ya AA si kweli, kuwa Abdul Sykes kadi yake no 3 si kweli kuwa kuwa kuwa...

Nini khasa hautaki kukisikia au ni cha uongo.

Kuwa Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika akizungumza na Abdul na Dossa na Nyerere ndani ya madrasa yake Mtaa wa Mvita ni uongo, kuwa alikuwa anauza kadi za TANU ndani ya misikiti si kweli.

Kuwa historia hii haikuwapo hadi Mohamed Said alipoiandika.
Nini khasa kinakutaabisha?

Kuwa unataka tuifute historia hii tubakie na ile ya zamani.
Nini khasa.
 
Imeina story imewaacha waislamu ndiyo maana ukaandika. Mzee huwezi kuwadangaya watu wote, Kwa miaka yote umekuwa unapromote waislamu ndiyo wenye Mchango pekee wa nchi hii! Lakini hakuna mtu aliyedhaminu historia hiyo maana hajabalance. Jipange upya
 
Hatuwezi wote tukawa waandishi ila haitunyimi nafasi ya kukosoa mtu anapotaka kupotosha umma.
Huna unachokosoa umejaa chuki tu.
Leteni ukweli hamna.

Kazi kulalamika tu. Anaandika waislamu tu, mlitaka aandike wasio kwenye historia ili abalance.

Historia ya uhuru hamuijui, mmelishwa matango pori kwa miaka mingi, eti mtu mmoja tu ndiye mpigania uhuru. Hakuna kitu kama hicho.

Wanatajwa wengine walioshiriki harakati za uhuru mnakasirika.

Tunashukuru sasa kizazi kimejua kuna wengine walioshiriki harakati za uhuru na si mtu mmoja.

Na kumbe watu walianza harakati kabla hajaja mjini.
 
Imeina story imewaacha waislamu ndiyo maana ukaandika. Mzee huwezi kuwadangaya watu wote, Kwa miaka yote umekuwa unapromote waislamu ndiyo wenye Mchango pekee wa nchi hii! Lakini hakuna mtu aliyedhaminu historia hiyo maana hajabalance. Jipange upya
Jesus,
Wakujipanga ni wewe.
Mimi nimeiandika historia ya TANU kama ilivyotakiwa.

Wewe sasa andika historia yako yenye balance.
 
Acha kutetea upuuzi. Au unalipwa na huyo mzee?
 
Anachofanya Mohamed Said kulazimisha "wazee wake" kuwa daraja moja sawa na Nyerere ni propoganda mbovu sana.
 
Anachofanya Mohamed Said kulazimisha "wazee wake" kuwa daraja moja sawa na Nyerere ni propoganda mbovu sana.
Yoda,
Ningejaribu kutia uongo katika historia ya Mwalimu Nyerere leo nisingefika katika kiwango hiki cha kuaminika kuwa naijua vyema historia yake.

Abdul Sykes na Hamza Mwapachu ndiyo watu wa karibu sana na Mwalimu ns siwezi kusema walikuwa sawa na yeye.

Nitasemaje hivyo ilhali wao waliujua uwezo wake na wakampa uongozi wa TAA mwaka 1953?

Wewe kuwa mkweli na nionyeshe wapi haya yameelezwa au wapi Nyerere kawaadhimisha wazalendo hawa wawili katika maisha yake?

Nimeshirikishwa katika miradi mitatu ya kuandika historia ya Mwalimu: Kitabu cha Jim Bailey wa Afrika Kusini, Nyerere Biography ya Shivji na wenzake na mradi wa historia ya Magufuli.

Ushindi wangu katika kuijua historia ya Nyerere uko wazi.

Vitabu viwili vya historia ya TANU vilivyowafuta watu kama Hamza Mwapachu na Abdul Sykes kitabu cha CCM Kivukoni na kitabu cha Abubakar Olotu vyote vimekufa.

Kitabu changu cha maisha ya Abdul Sykes miaka 25 leo kila uchao kipo midomoni mwetu tunakijadili.

Si hayo tu nimekizungumza kitabu changu katika vyuo vingi hadharani na pia katika faragha na wasomi mabingwa wa historia ya Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…