Andika kitabu tujifunze na tuone historia ya uhuru wa Tanganyika.Historia yako yote imeegemea kwa Sykes na uislamu kana kwamba hii nchi ilikuwa ya kiislamu. Maandiko yako karibu yote sijaona ukitaja jitihada zilizofanywa na mtu mwenye jina la kikristo. Hao wazungu waliokuita ukafanye mhadhara vyuoni kwao hawawezi kujua mambo yote yanayohusu nchi yetu. Hata mimi nikitaka kuandika kitabu kwa kusikiliza stori za babu zangu ninaweza. Kuna mzee wangu anaishi Ilala alikuwepo siku ya sherehe za uhuru 1961 na huwa ana mambo mengi sana ya kusimulia. USILAZIMISHE SIMULIZI ZA WAZEE WAKO NDO ZIKAWA MSIMAMO WA NCHI.
Naamini huwezi na hutaweza. Wameshindwa wenzio wengi walioahidi kufanya hivyo.
Wenzio waliokuwa wanampinga Mzee Mohamed Said na wameshindwa hoja,
huu uzi wanaupitia kimyakimya. Wenzio walipinga kwa hoja nzito lakini
mwisho walikimbia.
Kusimamia batili ni kazi ngumu sana.