Makosa ndani ya Makala ya Mama Maria Nyerere Kutimiza Miaka 93

Unajua sana hongera Baba yetu 🙏🙏🙏
 
Alipokelewa na kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes .........

Alikuwa na marafiki kina mama wa ukoo maarufu Kariakoo .........

Abdul Sykes na Ally Sykes walitoa mali na kila kitu kumsaidia Nyerere apate Uhuru.

Huyu babu wa kiislam ni aina ya watu ambao ambao akikusaidia UTAJUTA
 
Kwa vile katika Makala ile Sykes hakuandikwa
Naam,
Mtafiti yeyote atakae jaribu kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TAA, TANU na Mwalim Nyerere atakuwa ameacha sehemu kubwa na muhimu ya historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wako waliojaribu kufanya hivyo na ndiyo leo unaniona niko hapa naisomesha upya historia ya kupigania uhuru wa Tangnayika kwa makala na picha.
 
Mose...
Kanuni za uandishi ni kuweka dot 3 tu ...
 
Sasa kama alikuwa anauza soda kwa nini asiuze vitu vingine? Ndivyo ilivyokuwa maduka yetu ya mtaani wakati ule.
Hayo ya wakina Salim Ahmed Salim, Shivji na Mbita nimekuachia wewe kwa sababu hakuna hata mmoja wao ni historian. Kuwa na vitabu vingi au kuwa librarian hakukufanyi kuwa authority.

Unasema huna kawaida ya kumuita mtu muongo lakini maneno yako kuhusu hizi habari za duka la mama Maria ilikuwa inamuonyesha kuwa yeye ni muongo. Kumuita mtu muongo sio lazima utumie neno muongo.
Asante kwa picha zako pamoja na taarifa kuwa Bwana Rashaad Ali ni mzazi wako. Ni jambo jema.

Amandla...
 
Jazakallah Mzee kwa masahihisho🙏
 
Fundi...
Tumenufaika na taarifa kuwa Mama Maria pamoja na mafuta ya taa alikuwa anauza na Coca-Cola na jina la mtu aliyekuwa akimpelekea nimetajiwa.

Hili la Shvji kama nilivyokwisha kusema si lake.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kigoda Cha Mwalimu Nyerere taasisi ya taifa la Tanzania.

Niliwapa baadhi ya Nyaraka za Sykes na wakaniandikia kunishukuru.

Nyerere Foundation unawajua halikadhalika naamini unawajua Ford Foundation.

Labda usichokijua ni uhisuano wangu na taasisi hizi mbili.

Kigoda Cha Mwalimu na mimi tulikuwa karibu kidogo na licha ya nyaraka tumebadilishana fikra.

Nyaraka nilizowapa walikuwa wakizionyesha hadharani katika shughuli zao nyingi.
 
Hizo kanuni aliweka Mungu?

Hazibadiliki
Hizo kanuni aliweka Mungu?

Hazibadiliki
Mose...
Hapana hakuweka Mungu.
Zimewekwa na binadamu na wakifundisha shule.

Mathalan mwisho wa sentensi unaweka nukta.
Mwanzo wa sentensi unaanza na herufi kubwa.

Kwa kawaida sheria hizi hazibadiliki.

Fikra yangu nilidhani kuwa hujui nikaona nikifahamishe ili iwe unajua na hivyo kuongoza elimu yako.

Bahati mbaya inaelekea umeghadhibika kusahihishwa.
Niwie radhi.
 
Una matatizo mzee mwenzangu
 
Una matatizo mzee mwenzangu
Nafungua uzi mpya wa Sykes kuna mtu ameniuliza swali na wewe umenikejeli kuwa nina matatizo.

Ungeweza tu kueleza utakacho kiungwana bila ya kunitusi.

Ingia hapo chini tafadhali:

 
Hiyo makala yake anayosema anasahihisha makosa ya historia ya mama Maria Nyerere, ina makosa chungu nzima.
 
Kwa vile katika Makala ile Sykes hakuandikwa
Kolola,
Kipande muhimu kimerukwa kukosa kutaja kuwa Mwalimu alikaa kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley.

Akiwa hapo Mama Maria akafungua duka la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikichi.

Haikuelezwa kuwa walipohamia Magomeni Maduka Sita Mama Maria akapewa nafasi ya kuweka duka lake la mafuta nyumbani kwa Ali Msham.

Hii ni historia ya wazee wangu na ni jukumu langu kuhakikisha kuwa inahifadhiwa sawasawa.
 
Hivi unadhani kila kitu lazima kiandikwe? Unajua Nyerere aliolea kwa nani akiwa anafundisha Tabora? Huyo Sykes wako unamtukuza hadi unaboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…