Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Limekuwa jambo la kawaida sana siku hizi wasomaji wangu kuniletea taarifa nyingi ambazo wao wanazo katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Taarifa nyingine pamoja na picha zinatoka kutoka familia za wapigania uhuru ambao historia imewasahau.
Leo nimepokea picha ambazo kwa hakika zimenisaidia kuona kwa ndani zaidi hali ya jamii ya Moshi mjini ilikuwaje katika miaka ya 1950 wakati wa kupigania uhuru ingawa baadhi ya picha hizi zilipigwa uhuru ushapatikana.
Lakini juu ya haya ule mtandao wa akina mama bado upo haujavunjika.
Katika kitabu cha Abdul Sykes nilieleza kuwa TANU Moshi Mjini ilikuwa mikononi mwa akina mama na ni tawi pekee Tanganyika ambalo nguvu yake kubwa ilitokana na akina mama:
''Yusuf Olotu Yusuf labda kwa kuelewa mazingira ya Kilimanjaro alianza kujenga msingi wa TANU si kwa wanaume bali kutoka kwa akina mama.
Hiki ni kitu aziz sana katika historia ya uhuru.
Katika historia ya TANU ni zile sehemu ambazo kulikuwa na utamaduni wa Kiswahili wa vyama vya akina mama kama hapo Moshi mjini, Dar es Salaam, Tanga, Lindi na kwingineko ndiko chama kilipata nguvu kubwa sana ya wanawake.''
Wanawake wa Moshi Mjini, Mtaa wa Chini na Mtaa Juu na Majengo mila na utamaduni wao ni wa Kiswahili kabisa.
Nyimbo zinazoimbwa harusini ni zilezile zinazoimbwa Mombasa, Dar es Salaam, Lindi na sehemu nyingi za pwani.
Ila Moshi waliongeza ngoma ambayo kwa Tanzania naweza kusema inachezwa Moshi peke yake kwani haipo katika mji wowote Tanzania.
Ngoma hii inaitwa, ''Msanja.''
Nimeambiwa kuwa Msanja upo Mombasa na ndiko ulikotokea hadi kufika Moshi.
Ngoma hii huchezwa harusini na wanawake watupu na kwa kawaida huwa sehemu ile inapochezwa uwanja hufungwa yakazungushwa magunia kwa ajili ya stara kwa wanawake.
Wanawake huimba wakicheza na kupiga pembe za ng'ombe.
Katika picha nilizopokea ipo picha ya akina mama wakiwa harusini wengine wameshika pembe za ng'ombe.
Katika picha hii yuko Zena Maua mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Halikadhalika nimepokea picha ya Juma Ngoma mmoja wa waasisi wa TANU, Moshi.
Juma Ngoma nimemtaja katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Ilikuwa Yusuf Olotu ndiye aliyeweza kuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo mjini akaieneza vijijini.
Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf Olotu ndipo unapokutana na historia za awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo; na wengine kuwa mawaziri katika Tanganyika huru, kama Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.
Ilikuwa Yusuf Olotu ndiye pamoja na wazalendo wengine waliifanya TANU ishinde uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.
Kupitia kumbukumbu zake halikadhalika ndipo kwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe, mashujaa wa kike na wa kiume, wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, Amina Kinabo, Halima Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika na wengineo.
Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawala wa machifu (Mangi) wao na kujiweka chini ya TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.''
Juma Ngoma
Akina Mama wa Moshi Mjini
Bi. Zena Maua ni huyo nyuma ya Bi. Swalha mama mwenye miwani
Zena Maua
Yusuf Olotu
(Picha kutoka kitabu,''Uamuzi wa Busara,'' (2007)
Mwandishi Mohamed Said