DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Wenyeji wangu waliniambia kwa kuwa wao wako bize walilazimika kwenda kuwatafutia uanchama Watoto wao kwenye Maktaba ya Mkoa ili wapate nafasi ya kujisomea, lakini walichokutana nacho huko ni balaa.
Maktaba ni mbovu, mazingira nim abaya na siyo rafiki, ukiangalia ‘silingibodi’ zinaanguka, kuta zimebomoka sehemu kadhaa, kibaya zaidi sehemu ya kujisaidia Watoto choo ni kibovu.
Najiuliza hivi wahusika wa mkoa wanachukuliaje hali hiyo au wao wanaona kawaida tu jengo kuwa limechakaa vile, kwanza hata mtu huwezi kupata mudi ya kusoma.