Maktaba Yapokea Kalenda Inayoeleza Historia ya Ukombozi wa Afrika Kusini na Kitabu Kuhusu Ubaguzi Katika Elimu

Maktaba Yapokea Kalenda Inayoeleza Historia ya Ukombozi wa Afrika Kusini na Kitabu Kuhusu Ubaguzi Katika Elimu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
MAKTABA YAPOKEA KALENDA INAYOELEZA HISTORIA YA UKOMBOZI WA AFRIKA KUSINI NA KITABU KUHUSU UBAGUZI KATIKA ELIMU

Mmoja wa wapenzi walio mstari wa mbele katika kuitia nguvu Maktaba ameitunuku calendar na kitabu.

Ingawa kalenda imekuja katikati ya mwaka lakini haikuwa shida kubwa kwangu kutambua kwa nini muhisani huyu aliona ni lazima kalenda hiyo aifikishe Maktaba.

Kalenda hii kwa hakika umuhimu wake si katika kuonyesha siku za miezi katika mwaka mzima.

La hasha.

Kalenda hii imekusudiwa kuhifadhi na kukumbusha kipindi chote cha mwaka mzima historia ya wazalendo waliopigania ukombozi wa Afrika ya Kusini dhidi ya Makaburu katili.

Ndani ya kalenda hii kumbukumbu ya wazalendo hawa imewekwa katika picha na maelezo muhimu ya kihistoria katika yale yaliyotokea nchini.

Kalenda ina picha ya Mauaji ya Sharpeville ya mwaka wa 1960.

Hili ni tukio muhimu katika kalenda ya makubwa yaliyotokea Afrika ya Kusini.

Wakati hata fikra hazijahama kwenye tukio hili ukurasa wa kalenda unaonyesha picha ya mistari mirefu ya wananchi wakisubiri kupiga kura Uchaguzi Mkuu wa kwanza Afrika ya Kusini mwaka wa 1994.

Kuna picha ya marehemu Albert Luthuli aliyekuwa Rais wa African National Congress na mshindi wa Nobel Peace Prize mwaka wa 1961.

Sikuendelea kufungua kalenda hii nikaifunga nikatuliza kichwa changu nikajiuliza itakuwaje kama nasi tutatengeneza kalenda kama hii na tukaweka picha za mashujaa wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika hasa wale ambao hawafahamiki sana.

Hawa ni wale wazalendo historia imewasahau.

Fikiria unafungua kalenda unaona picha ya Ali Migeyo wa Kamachumu, Awadh Msham wa Mikindani, Ali Msham wa Magomeni Mapipa Dar es Salaam, Sheikh Mohamed Yusuf Badi wa Lindi, Bi. Aza wa Kilwa, Bi. Shariffa bint Mzee wa Lindi, Mohamed Mangiringiri wa Tabora, Ismail Bayumi wa Moshi kwa kuwataja wachache.

Fikiria unatazama picha na unasoma historia zao.

Hakika wazalendo hawa wa kuingia kwenye kalenda ya Tanganyika ni wengi sana na historia zao zinasisimua.

Fikra hii yangu inanisisimua kama historia hizi zinavyovutia.

Mshauri wangu nimemueleza fikra hii.

Yeye kapanua wigo anasema jitihada ifanywe asibakishwe mzalendo yeyote nje wote waonekane ndani ya kalenda.

Nami ikanijia wazo kuwa kalenda ionyeshe na nyumba ambazo watu waijitolea kuzifanya ofisi na matawi ya TANU.

Halikadhalika zionyeshwe nyumba alizokuwa akilala Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika majimbo na vitu vingine mfano pikipiki ya Abdulkarim Hajj Mussa Jemadari aliyokuwa akimpakia Mwalimu kumtembeza Kilwa yote na nyumba ya Mwinyi Mcheni Omari aliyokuwa akilala na nyumba ya Ahmed Adam Mikindani aliyolala Mwalimu safari yake ya kwanza Southern Province.

Mshauri ananitia moyo anasema si kazi ngumu kwani hapa tutatengeneza urithi kwa vizazi vijavyo.

1783795737305.png
1783795822786.png
1783795864128.png
1783795893399.png
1783795913527.png
1783795945243.png
 
Sikuendelea kufungua kalenda hii nikaifunga nikatuliza kichwa changu nikajiuliza itakuwaje kama nasi tutatengeneza kalenda kama hii na tukaweka picha za mashujaa wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika hasa wale ambao hawafahamiki sana.

Hawa ni wale wazalendo historia imewasahau.

Fikiria unatazama picha na unasoma historia zao.

Hakika wazalendo hawa wa kuingia kwenye kalenda ya Tanganyika ni wengi sana na historia zao zinasisimua.

Nami ikanijia wazo kuwa kalenda ionyeshe na nyumba ambazo watu waijitolea kuzifanya ofisi na matawi ya TANU.

Mshauri ananitia moyo anasema si kazi ngumu kwani hapa tutatengeneza urithi kwa vizazi vijavyo.
Asante kwa uzi huu.
P
 
Back
Top Bottom