Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nawashukuru ndugu zangu kupita kiasi.
Kila siku wananikumbuka na kuniletea vitabu ama wavitume au kuja wenyewe maktaba kwa miguu yao.
Abdulaziz Ali Khamis yeye anatoka Mombasa.
Mara kwa mara huja nitembelea Maktaba.
Safari hii alikuja Tanzania akafika hadi Songea kutembelea Makumbusho ya Vita Vya Maji Maji.
Hapo kuna duka la vitabu basi akaninunulia kizigo cha vitabu kaniletea.
Kitabu kilichogusa moyo wangu ni hicho nilichoshika kitabu cha Nduna Abdulrauf Songea Mbano kiongozi wa Wangoni.
Wanahistoria hupenda kumwita Songea Mbano wakaliacha jina la Abdulrauf.
Mimi hupenda kumwita kwa majina yake kamili: Nduna Abdulrauf Songea Mbano.
Alinyongwa na Wajerumani na kukata kichwa chake wakakipeleka Ujerumani.
Ndugu yangu Mohammed Abdulrahman, somo yangu na mwanaKariakoo mwenzangu nguli wa utangazaji sihitaji kumweleza sana.
Mohammed kapinda mgongo kaandika kitabu cha maisha yake.
Majuzi kanituliza.
Kanambia nitulie nikimalize kitabu kwani maswali ninayomvurumishia mbona yote majibu yamo kitabuni?
Nina wahka.
Nashindwa kutulia.
Mohammed ni kamusi kubwa ya historia ya kudai uhuru wa Ngazija.
Nilijua hili miaka michache iliyopita nilipoandika taazia ya rafiki yangu Salim Himidi aliyefariki Paris.
Aliniletea picha na maelezo mengi.
Katika kitabu hiki nina deni kubwa lazima In Shaa Allah nililipe.
Kitabu kinanidai pitio.
Bi. Zawadi Sakapala wa Mtoni Kijichi na Washington DC leo kaniletea mabuku makubwa matatu.
Naamini kabisa kwenye ndege mzigo huu wenye uzito wa nusu mfuko wa sementi umemgharimu.
Yote historia ya Marekani ya kale na leo. Namshukuru sana kupita kiasi.
Buku moja kaandika Peter Jennings nguli katika utangazaji Marekani, alikuwa Anchor wa ABC News.
Sasa ni marehemu.
Sapakala ni katika koo kubwa za Dar-es-Salaam ingawa hawavumi.
Lakini ukifika Mtoni Kijichi utawajua.
Wamejenga kituo kikubwa cha elimu kwa watoto wa Mtoni.
Huu ni mfano mkubwa wa kuigwa na wote ambao Allah kawaneemesha.
Ukoo wa Sakapala wamevunja nyumba moja ya baba yao kujenga kituo hicho na kila mwaka anakuja na timu ya wanaelimu kutoka Marekani kuja kujifunza historia na utamaduni wa Watanzania waishio Mtoni.
Hakika ndugu zangu wote hawa watatu wamenifurahisha nami namuomba Allah awafurahishe kama walivyonifurahisha mimi.