Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Ndugu kuna baadhi ya Madaktari hasa hawa Clinical officer huwa hawajielewi kabisa kwa hiyo bila kutafuta maarifa ya ziada na kujisomea wanaweza kukuadhiri, mama yangu aliwawi kuandikiwa dawa ambayo wajawazito hawaruhusiwi kuitumia pindi yupo mjamzito ikapelekea kujifungua mtoto mfu, nimekuja kujua hili baada ya kukua uzuri Maza hakusahau jina la ile dawa hadi leo.
Kuna rafiki yangu mama yake alikuwa na kisukari au complications fulani sikumbuki ila inatakiwa akiwekewa drip kuna aina maalum vinginevyo mgonjwa anakufa. Siku hio mama yao mgonjwa hajitambui wamempeleka hospital nurse akawa anamtundika drip ya kawaida. Rafiki yangu na dada yake katika umri mdogo sana walimgonea yule nurse ndio kuja kuangalia ni kweli hatakiwi kuwekewa drip ya kawaida. Bila wao kuwa na uelewa wa hali ya mama yao huyo nesi angemuua kizembe. Kwahio sometimes medical professionals huwa wanakosea
 
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Waliochukua mchepuo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.

- Wenye followers kuanzia elfu 20, 30, 40 au zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kma wewe sio star usitegemee kama atakufollow back.

- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Vijana wa kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi bongo kupambana na msoto wa maisha.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira jeshini halafu uwakute uraiani wamevaa zile gwanda zao.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
Wanaotembea na wasanii.
 
Kuna majamaa flani jioni jioni utawaona wana kopo la maji ya kilimanjaro wamevaa vi pensi vya khaki na mashati ya form six.. mikononi wameshika simu kubwa huku wamening'iniza funguo kwenye luxi ya kaptula..
Hawa wanaona maisha wameyapatia kabisa
Nimecheka sana hao wanapatikana kwetu pazuri na forty forty TABATA
 
Unaonekana unawatazama sana watu mkuu
Hadi ukaweza kuwachambua hivyo, sijui utakuwa na kazi gani
Kwakweli inahitaji muda akili na nguvu nyingi sana aisee..

Yani hadi mtu anakuja na Uzi huu..

Hakika ana muda..
 
Du hawa huwa wako sana mitaani karibu na baa mpya siku za Ijumaa hadi Jumapili mida ya jioni
Kuna majamaa flani jioni jioni utawaona wana kopo la maji ya kilimanjaro wamevaa vi pensi vya khaki na mashati ya form six.. mikononi wameshika simu kubwa huku wamening'iniza funguo kwenye luxi ya kaptula..
Hawa wanaona maisha wameyapatia kabisa
 
Mimi siyo mmojawao ni veteran tu humu. Ila Sijaelewa kwanini tunasema wanajidai wamepatia sana maisha . Watu walitakaje? Hao tunaowasema wanajipima kwa vipimo vyao wenyewe na hiyo kwao ni sawa.
JK aliwahi sema " raha jipe mwenyewe"

Mtu anaamua kujitutumua kwa kuamini ame win maisha kwa vigezo vyake. Ni hatari kusubiri mtu akusifiye ndo useme umetoka kimaisha;some time watataka kukulinganisha na akina Mengi, Bakhresa, Manji nk ukijua huko hutaweza kufika. ili uwe na raha ni bora tu ujiaminishe kuwa nimiko saafi. Some time wapambe humpotosha mtu hivyo ni bora ukatoka kivyako tu. Huu ni mtazamo wangu
 
Members wengi wa JF wanajiona wameyapatia maisha na kudharau platform nyingine kama FB,. NOTE; Hakuna aliyekamilika, Ishi uhalisia wa maisha yako usipende kujaji watu bila sababu za msingi,.. Nacomment kupitia iPhone X.
Utaskia "ebu peleka huu ujinga kwa watoto wenzio huko FB"

Wanafurahishaga sana
 
Nimesubscribe huu uzi njionee kama tabia zangu zikoje ktk macho ya watu
 
Utaskia "ebu peleka huu ujinga kwa watoto wenzio huko FB"

Wanafurahishaga sana
Hahahahaaa ChickMagnet,.. kuna haka ka msemo ka kizhuuungu "Smarter People underestimate themselves, Ignorant people think they`re brilliant". Sasa wanaanzaje kuita wenzao wajinga kama wao sio wajinga.
 
Back
Top Bottom