RoadLofa
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 1,509
- 3,313
Machalii wa rMachalii wanaosuka rasta ili wapate vibibi vya kizungu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Machalii wa rMachalii wanaosuka rasta ili wapate vibibi vya kizungu.
kwahiyo mkuu kilicho kuuma ni demu wangu kuweka miguu juu ya dashboard au mimi kukumwagia maji kwa bahati mbaya?.................Mkuu bora umeanzisha huu uzi hapa.
Juzi jumamosi nikiwa natoka home na mvua hizi maji yametuama hovyo naelekea stand za huku mitaani maeneo ya Mbezi Kimara bwana mdogo mmoja yupo na gari yake Mazda model siikumbuki ila ni hizi saloons za 9.7/10.5mill mimi napita pembeni mwa barabara huku nazungumza na simu sina hili wala lile mara pwaa!
Mimaji michafu suruali yote mpaka raba nilizokuwa nimevaa zimebadilika rangi zimekuwa tope na nilivaa cadet ya khaki simple nyeusi na nyeupe,wala hakujali na sababu barabara ina mashimo alikuwa anaenda speed ndogo sana but alishindwa hata kushusha kioo kuniambia samahani nachokumbuka aligeuka kidharau akanitazama kisha huyoo akenda zake huku seat ya kushoto amekaa mwanamke wake ameweka miguu kwenye dushboard wala hawakujali.
Sehemu yenyewe ni karibu na CCM wanakolaza magari sasa jamaa waliokuwa wamekaa pale picha waliiona wakaniambia bwana huyu jamaa gari yake huwa inalalaga hapa yeye kapanga kwenye nyumba ile palee!nikajisemea kimoyo moyo hakika Tanzania ukiwa na gari wewe ndo tajiri yaani amepanga chumba na sebule ananimwagia mimi maji machafu hata haonyeshi ubinaadam?any way niliacha likapita ila siyo vizuri tusidharauliane sana tunapohisi tuna mafanikio fulani wakati mwengine unaemdharau anaweza kuwa amekuacha mbali sana wanojua wakakucheka.
Hujakutana na dereva bajaji aliemaliza mkataba, huwa wanajikuta wanaimiliki dunia
Pole mkuu...Ndugu kuna baadhi ya Madaktari hasa hawa Clinical officer huwa hawajielewi kabisa kwa hiyo bila kutafuta maarifa ya ziada na kujisomea wanaweza kukuadhiri, mama yangu aliwawi kuandikiwa dawa ambayo wajawazito hawaruhusiwi kuitumia pindi yupo mjamzito ikapelekea kujifungua mtoto mfu, nimekuja kujua hili baada ya kukua uzuri Maza hakusahau jina la ile dawa hadi leo.
😀😀😀😀😀😀😀 nimekaa nao sana hao JW yaani sie ambao sio askari wanatuona yaani kama chokoraa,nadhani ni kutokana na spirit wanayomezeshwa kipindi cha mafunzo ndio inayowajenga KUJIMWAMBAFY.,.....Mwanajeshi bora umtukane matusi mengine lakini kamwe usijaribu kumwita "RAIA".Hapa sasa hivi katoka kulitumia😂😂 Anamwambia mama Ile sio kambi ile Combania we utajuaje wakati wewe "Raia" 😂mama anamjulia nae kamjibu iwe kombania au komba ngurue mtajijua wenyewe
Atakuua😂😀😀😀😀😀😀😀 nimekaa nao sana hao JW yaani sie ambao sio askari wanatuona yaani kama chokoraa,nadhani ni kutokana na spirit wanayomezeshwa kipindi cha mafunzo ndio inayowajenga KUJIMWAMBAFY.,.....Mwanajeshi bora umtukane matusi mengine lakini kamwe usijaribu kumwita "RAIA".
Hahahaaaa wanajeshi wakionana wanaitana "WAPOTI".Atakuua😂
Ngoja kesho nimchokoze wapoti nimwambie baba we si Raia tu
Ukiona kimya uje mloganzila kuniona mkuu
Wengi wa Musoma "poti" 😂Hahahaaaa wanajeshi wakionana wanaitana "WAPOTI".
Don't compare Jf and other social networks.... tafadhali mkuu hii ni zaidi ya social media...ipe heshima yake na unatakiwa uombe radhiUnaizungumzia JF ipi mkuu?
JF hii ambayo topic ya kula mademu kimasihara inapata page 50 kwa siku mbili tu?
Unazingumzia JF ipi ambayo hakuna mashoga na makahaba
Jf ipi ambayo ni tofauti na fb,instagram na twitter?
Sikiliza mzee labda tofauti huku hatutupii picha zetu
Ila ujinga wa social media ni ule ule
Kyusa poti pia 😂😂😂Wengi wa Musoma "poti" 😂
Live your life to the fully,acha wajidai,maisha ni haya haya,we live once- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.
- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Waliochukua mchepuo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.
- Wenye followers kuanzia elfu 20, 30, 40 au zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kma wewe sio star usitegemee kama atakufollow back.
- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.
- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.
- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.
- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira jeshini halafu uwakute uraiani wamevaa zile gwanda zao.
Ongezea wengine unaowajua.
Karibuni.
[emoji23][emoji23]Wale jamaa wanaokaa bar na laptop zao na maji makubwa Kwa pembeni. ...