Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

Don't compare Jf and other social networks.... tafadhali mkuu hii ni zaidi ya social media...ipe heshima yake na unatakiwa uombe radhi

Mkuu wewe ni member since 2014


Mimi ni member since 2012 hatuna gap sana toka tuanze kutumia JF

Hebu niambie tofauti ya JF na social media zingine ni nini?

Huenda kweli nakosea
 
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Waliochukua mchepuo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.

- Wenye followers kuanzia elfu 20, 30, 40 au zaidi kwenye mtandao wa Instagram. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kma wewe sio star usitegemee kama atakufollow back.

- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira jeshini halafu uwakute uraiani wamevaa zile gwanda zao.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
POLISI.....
 
Soon Twitter inakua kama Instagram na facebook. Zamani twitter ilikua inachukuliwa kama platform ya elites kujadili mambo ya kitaifa na mambo magumu, leo kule twitter ni umalaya, ukahaba, ushoga, ujinga. Watu wanajadili mambo ya hovyo.

Nadhani platform pekee iliyobaki ya kuchangia mambo ya maana ni JF kwa sababu imetutengea majukwaa, kila mtu anachangia jukwa ambalo akili yake inaweza kujadili.
mkuu sio soon twitter sasa hivi utofauti wa na insta ni picha tu.
 
mwenye geto na mkononi ana simu yake kubwa matoleo mapya mapya,au anae miliki boda boda
 
Tanzania umaskini wa akili ni mkubwa sana. Hapo akisimamishwa kazi mwezi mmoja tu anapata fistula hata kama ni wa kiume.
Sawa Wewe Ndio Tajiri Wa Akili, Usiyejua Kuwa Hata Wanaume Wanapata Fistula
 
Kuna rafiki yangu mama yake alikuwa na kisukari au complications fulani sikumbuki ila inatakiwa akiwekewa drip kuna aina maalum vinginevyo mgonjwa anakufa. Siku hio mama yao mgonjwa hajitambui wamempeleka hospital nurse akawa anamtundika drip ya kawaida. Rafiki yangu na dada yake katika umri mdogo sana walimgonea yule nurse ndio kuja kuangalia ni kweli hatakiwi kuwekewa drip ya kawaida. Bila wao kuwa na uelewa wa hali ya mama yao huyo nesi angemuua kizembe. Kwahio sometimes medical professionals huwa wanakosea
Hiyo Ilikuwa Ni Diabetic Ketoacidosis Na Nurse Baada Ya Kumpa Normal Saline Alitaka Kumpa Ringer Lactate Lazima Angemuua.

Muda Mwingine Nurses Hawajui Vitu Wanafanya Kwa Mazoea Na Kuona Dr Kafanya Order.
 
Hiyo Ilikuwa Ni Diabetic Ketoacidosis Na Nurse Baada Ya Kumpa Normal Saline Alitaka Kumpa Ringer Lactate Lazima Angemuua.

Muda Mwingine Nurses Hawajui Vitu Wanafanya Kwa Mazoea Na Kuona Dr Kafanya Order.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Mkuu unasema Watanzania wengi kwa vile umeishi nao sana au? je unajua wengine uko wakoje? USA,China,Australia n.k?
UKISOMA HII TOPIC NA MICHANGO YAKE NDIO UTAJUA AKILI ZA WATANZANI WENGI.

UTAONA JINSI WATU WALIVYO BUSY KUCHUNGUZA MAISHA YA WATU NA KUANZA KUWA-JUDGE.

WATANZANIA WENGI WAMEJAA WIVU, MAJUNGU NA UCHUNGUU MWINGI NDANI YA MIOYO YAO.

MFANO, MTU AKINUNUA VITZ AU IST WEWE ANAKUKERA NINI?
 
Walevi aisee wana raha sana nahisi ndio kundi ambalo limepatia maisha sizungumzii wanywaji ila walevi hawanaga stress kabisa
 
Kuna majamaa flani jioni jioni utawaona wana kopo la maji ya Kilimanjaro wamevaa vipensi vya khaki na mashati ya "form six" mikononi wameshika simu kubwa huku wamening'iniza funguo kwenye luksi ya kaptula.

Hawa wanaona maisha wameyapatia kabisa.
Nawashangaa sana hawa vijana,miadi yao mingi ni ya kula starehe. Wanaishi kwa kukopa kopa ili kuonyesha hawajatetereka
 
Wanaopenda kwenda Samaki samaki na 777 na joints za Mikocheni na Masaki
 
Kwa waliojenga nyumba kiasi wamepiga hatua mkuu
Nadhani ni wajita wao wanasema kama mwanaume una umri mkubwa na una mademu 20, bado ni mtoto kuliko kivulana chenye miaka 18 na mke mmoja. Hata kama unafanya kazi benki kuu lakini unaishi nyumba ya kupanga, mpiga debe mwenye nyumba mbavu za mbwa ni bora zaidi.
 
Nani aliyekwambia tunakwazika wewe wana nini cha ziada huwa tunawachora tu mana wengi wanajifanya matawi ya juu
Jifunze ku-mind your business.

Huko kuwachora ni ushamba na ulimbukeni, tafuta hela usifuatilie maisha ya wenzako.

Poverty striken minds.
 
Back
Top Bottom