Makusanyo ya Kodi kupanda kutoka trilioni 1.2, mpaka trilioni 2 awamu ya 6, ni nani hawa walikuwa wanakwepa Kodi ya bilioni 800 Kila mwezi?

Makusanyo ya Kodi kupanda kutoka trilioni 1.2, mpaka trilioni 2 awamu ya 6, ni nani hawa walikuwa wanakwepa Kodi ya bilioni 800 Kila mwezi?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Samia Suluhu Hassan katika makusanyo ya Kodi, amepanda kutoka trilioni 1.2 mpaka trilioni 2, swali la kujiuliza, hii Kodi ya bilioni 800 nani alikuwa anakwepa kuilipa?

Na je akibanwa? Tunatarajia hatapiga au hawatapiga yowe? Piga hesabu bilioni 800 zilikuwa haziingii hazina zikajenge mahospitali, mashule, mabarabara.

Mtu akiwakazia watu waliokuwa wanakwepa Kodi na kuwabana ni mzalendo, Sasa mfuko wa hazina unatuna, nadhani ni WA kumpongeza .....au tumkatishe tamaa turudi kwenye trilioni moja?

Halafu wanaokwepa kodi, tunakutana nao kitaa hata bia hawatupi, wanatuona malofa, si Bora walipe Kodi ijenge lami tupite wote, wao kwa benzi sisi kwa daladala? Kuliko hawalipi Kodi, wanaturushia tope barabarani na lift hawatupi

Kodi kwa maendeleo ya taifa
 
Kama anakusanya til. 2 kwa mwezi kwanini kakopa til. 30 ndani ya miaka 2?

Haya mahel yote yanaenda wapi?
 
Rushwa zote zinazoenda kwa maafisa zikibanwa zikaenda serikalini zitapanda.
 
Kilichofanyika kikubwa nikuongeza idadi ya walipa Kodi kwa kuvutia wawekezaji wengi na kuhamasisha wafanyabiashara wazawa waliokombiza mitaji Yao nje ya nchi warudi kufanya biashara zao nyumbani.kwa kufanya hivyo ongezeko la makusanyo lazima llionekane.
Walichofanya wameongeza kodi lukuki za kuwakamua watanzania ndiyo maana maana makusanyo yanaonekana yameongezeka.
 
Usikute hakuna hata anayekwepa, isipokuwa kilichokngezwa ni pamoja na Tozo, Kulipia Mita luku n.k

Lakini pia, kwa miaka miwili, kuna biashara zinaongezeka n.k

Kwanza ni kiasi kidogo sana kulichoongezeka kwa makusanyo ya kodi ukilinganisha na utitiri wa kodi mpya

Kwa mjibu wa nchemba waziri wa fedha, baada tu ya kuweka tozo kwenye miamala ya simu tofauti na miamala ya kibenki, kwa mwizi mmoja alikusanya bilioni 300+

Sasa kama ni hivyo, wewe unaona maajabu ongezeko la 800b?
 
Back
Top Bottom