Hawawezi kutusahaulisha, bandari zetu watanganyika ni haki yetu, tena bila kujali matokeo yoyote ya hukumu ya kesi itakayotajwa kesho mahakamani Mbeya.
Bandari zetu ni haki yetu, tuliachiwa urithi na wazee wetu, nasi ni jukumu letu kuzilinda. Kesho iwe iwavyo, haki ya mtanganyika kumiliki rasilimali aliyopewa bure na muumba itaendelea kubaki pale pale, haki hiyo haipo mahakamani.
Mahakamani walienda kutafsiri sheria pekee, lakini haki ya umiliki wa bandari zetu imetoka kwa muumba wetu, aliyeziumba mbingu na ardhi, na wala sio hakimu wa mahakamani.