Najiuliza, kama kila mtu katika hizi zama amekuwa mgumu kukubaliana na habari za watu wanaojiita manabii
Ilikuwaje kipindi cha nyuma watu wa enzi hizo kuwe na urahisi wa kuwakubali manabii wa kipindi hicho, ambao wakasababisha kizazi hiki kikarithi tabia hiyo?
Kizizi hiki kwa utashi ambao kipo nao leo, kingepata bahati ya kukutana na hao manabii wa kipindi hicho naona isingekuwa rahisi kuwaamini hao manabii ambao leo wanaaminiwa kutokana na kurithishwa. Watu wamerithishwa imani kua kuna Yesu, petro, muhammad, maria, nk.
Nikianza kuangalia yule yesu aliyekuja mwaka juzi hapo kenya na still watu wakamkataa napata hofu kwamba kuna siku hata akija huyo yesu na akajitambulisha kwamba yeye ndio yesu OG watu mtamkataa kwa kutumia vifungu vyake alivyoviandika yeye mwenyewe kua manabii wengi wa uongo watakuja kwa jina langu