Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

kiduni

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2015
Posts
348
Reaction score
341
Ongezeko jipya la bei za vifurushi bila shaka ni matokeo ya mazungumzo baina ya waziri mwenye dhamana na wamiliki wa mitandao ya simu.

Tuoneshe kupinga kwa vitendo tusinunue vocha tuziache simu zetu hewani bila vocha mpaka pale watakaposhusha gharama za vifurushi tunaumizwa kwa kweli.

Wenye mitandao watakosa fedha na hiyo itapelekea hata serikali kukosa fedha ambazo wanapata kama kodi lazima watakaa chini kuangalia upya vifurushi vya simu lakini kama tutakua tunalalamika halafu tunaendelea kununua vifurushi vyao hawatahangaika na sisi.
 
Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....

Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Hii tuifanye kampeni ili tupate unafuu wanatuita wanyonge ili tunyongwe hawayajui maumivu yetu
 
Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....

Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Ingewezekana kama kuna mbadala wa mawasiliano, lakini kuvimba kichwa bila mbadala haitawezekana hata kidogo.
 
Hii meseji ya kuhamashisha mgomo wa kununua vocha umetumia kifurushi (vocha) au umetumia hewa kuituma humu ndani??!!
Ndiyo sasa utoe wazo mbadala kama unaona hili ongezeko la bei ya vifurushi linakugusa
 
Back
Top Bottom