Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Malalamiko hayatoshi tusinunue vocha

Wabongo ni macoward sana muda mwingine.....

Nasema sisi wanunua vocha tukiuchuna japo kwa siku 30 tu..... Utakuja kuona hiyo simu kama ndani ya wiki moja hawatakaa kurekebisha vifurushi na kurejesha vile tunataka....
Ukitaka ujue level ya unafki ilipofikia hapa bongo. hakuna atakaye jaribu kufanya hiyo kitu.
Malalamiko kibao lakini msimamo hakuna.
 
Ushauri wako hautekelezeki bwashee!
Kwenye huu mgomo, tutaishia tu kusalitiana. Jambo la msingi Serikali iangalie kilio cha raia wake. Kama hakuna ulazima wa kuwaumiza, warudishe tu utaratibu kama zamani.

Ila kususia kabisa, sidhani! Mawasiliano kwa sasa ni jambo muhimu sana. Ingekuwa ni miaka ile ya 1990's tungeweza.
 
Tatizo ni shida ndo zitakazotuponza kununua vocha, ila Ndugulile ni fala mmoja anayetutesa Watz wenzake[emoji3525][emoji3525][emoji3525]
 
Ila huyu waziri katukosea Sana wapiga kura! Tumemtuma jikoni akaongeze mboga kaenda kujipendekeza kwa mpishi karudi na Bakuli la mchuzi, Bora angerudi na zilezile finyango zetu tano za minofu.

[emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi vocha nitanunua na bando nitajiunga. Kwanza niseme wazi Bei iongezeke maradufu wajinga wapungue mitandaoni
Mtu yupo tayari ashinde njaa ila aweke vocha. Maisha tu yatakuwa magumu lkn mitandaoni watu wataingia Kama kawaida
 
Back
Top Bottom