A
Anonymous
Guest
Vijana tupatao 436 tuliowahi kuahidiwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwamba baada ya kumaliza mafunzo yetu tungeajiriwa moja kwa moja, hadi sasa hatujaajiriwa wote.
Baadhi yetu tumebaki mitaani bila ajira, huku wengine wakiwa wanakabiliwa na changamoto za kiafya. Wapo pia waliojeruhiwa wakati wa kutekeleza majukumu yao na kupata ulemavu au majeraha ya kudumu.
Tunaomba Serikali ilifanyie kazi suala hili na kuangalia uwezekano wa kutekeleza ahadi hiyo, kwa kuzingatia vijana tulijitolea, tukafanya mafunzo na kutekeleza majukumu kwa imani kwamba tungepata ajira baada ya kukamilisha mchakato huo.
Pia soma ~ JKT waliojenga Ikulu ya Chamwino na kudai kutelekezwa, wamekutana na Waziri Dkt. Rhimo Nyansaho