A
Nina wafahamu vijana kama watatu waliopitia hii Kadhia huwa najisikia vibaya sana nikionana nao mtaani mmoja nipo nae mtaan yaan ni kama hana Dira kabisaMimi ni miongoni mwa vijana 436 tuliojenga Ikulu ya Chamwino lakini hatujapatiwa ajira kama ahadi ilivyokuwa, sasa wengi wetu tunaumwa mgongo, bawasili na kifua vyote vimetokana na kazi hiyo.
Ujumbe huu ufike Serikali Kuu ili watusaidie japo kutibiwa au kufanyiwa checkup, wenzangu wengine wamelazwa hospitali.
Tulipewa nafasi hiyo ya ujenzi na Rais Magufuli ambaye pia alikuja location akatamka kuwa tukimaliza ujenzi vijana wote 2000 tupewe ajira Jeshini.
Tulishaandika barua kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri Mkuu (kipindi kile yupo Majaliwa) kuhusu maombi yetu kupata ajira au kusaidiwa lakini hatujapata msaada mpaka sasa.