Malalamiko kuhusu dai la faini kwa abiria wa SGR

A

Anonymous

Guest
Leo, Oktoba 10, 2026, mimi na ndugu yangu tulisafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro, katika behewa namba 14, siti namba 41 na 42.

Wakati wa kukata tiketi, tulifanya makosa kwa kukata tiketi mbili zenye jina moja. Hata hivyo, tulifanikiwa kutatua changamoto hiyo na kupanda treni.

Changamoto ilijitokeza pale mmoja wa wahudumu wa SGR anayekagua tiketi alipokuja na kudai kwamba tulipaswa kulipa faini ya mara mbili ya nauli, ambayo ni Sh45,000, ikilinganishwa na nauli ya Sh22,500. Alidai kwamba tusipolipa, hatungeruhusiwa kushuka Morogoro.

Nilipomuomba anipatie namba ya malipo (control number) ili tulipe faini hiyo kupitia utaratibu rasmi, alidai kuwa hawatoi control number na badala yake akatutaka tutume fedha kwenye namba yake ya simu.

Swali langu ni hili: Je, utaratibu huu ni sahihi? Ikiwa faini hiyo ni halali, kwa nini malipo yafanyike kupitia namba binafsi ya simu badala ya utaratibu rasmi wa malipo?

Naiomba Shirika la Reli Tanzania (TRC) lifafanue suala hili ili abiria wafahamu utaratibu sahihi wa kulipa faini na kuepuka uwezekano wa kudaiwa fedha bila uthibitisho rasmi.
 
Kwahiyo na wewe ukalipa kwa kutumia namba yake binafsi...?
 
Yaani hakuna kitu kama hicho, kama umeshapanda kwa utaratibu halali waliokupa, hawana haki ya kufanya detainment yoyote
 
Leo, Oktoba 10, 2026, mimi na ndugu yangu tulisafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro, katika behewa namba 14, siti namba 41 na 42.

Wakati wa kukata tiketi, tulifanya makosa kwa kukata tiketi mbili zenye jina moja. Hata hivyo, tulifanikiwa kutatua changamoto hiyo na kupanda treni.

Changamoto ilijitokeza pale mmoja wa wahudumu wa SGR anayekagua tiketi alipokuja na kudai kwamba tulipaswa kulipa faini ya mara mbili ya nauli, ambayo ni Sh45,000, ikilinganishwa na nauli ya Sh22,500. Alidai kwamba tusipolipa, hatungeruhusiwa kushuka Morogoro.

Nilipomuomba anipatie namba ya malipo (control number) ili tulipe faini hiyo kupitia utaratibu rasmi, alidai kuwa hawatoi control number na badala yake akatutaka tutume fedha kwenye namba yake ya simu.

Swali langu ni hili: Je, utaratibu huu ni sahihi? Ikiwa faini hiyo ni halali, kwa nini malipo yafanyike kupitia namba binafsi ya simu badala ya utaratibu rasmi wa malipo?

Naiomba Shirika la Reli Tanzania (TRC) lifafanue suala hili ili abiria wafahamu utaratibu sahihi wa kulipa faini na kuepuka uwezekano wa kudaiwa fedha bila uthibitisho rasmi.
Kwahiyo mlizuiwa kweli kushuka au ukalipa kwa no yake ya simu?.
 
ulifanya jambo la maana ana kuomba control number, na siku nyingine usiishie tu kuomba control number, omba pia na reference ya hiyo faini anatoa wapi
 
Back
Top Bottom