A
Anonymous
Guest
Habari wadau,
Ninaomba kutoa lalamiko langu kuhusu huduma za masomo kupitia Zoom lectures zinazotolewa na Open University Tanzania kwa wanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza (bachelor of Laws) na wengine.
Tatizo kubwa ni kutokufundishwa kwa wakati kupitia Zoom lectures. Mara ya mwisho kufundishwa kupitia Zoom lectures ilikuwa mwezi wa tano mwaka huu (2024) kwa kila somo.
Hadi sasa, hatujapewa ratiba nyingine ya vipindi vya Zoom kwa muda mrefu, hali ambayo inatuletea changamoto kubwa katika kujifunza na kuelewa masomo
Ombi langu:
Tunaiomba taasisi ya Open University Tanzania itatue tatizo hili haraka iwezekanavyo. Vipindi vya Zoom ni muhimu sana kwa sababu vinatusaidia kuelewa masomo yetu na kutusaidia kujisomea wenyewe kwa ufanisi zaidi.
Naomba uongozi wa Open University Tanzania uchukue hatua stahiki ili kuhakikisha tunapata elimu bora na ya wakati.
Ahsanteni.