Msemaukwelii
Member
- Mar 20, 2017
- 9
- 3
Kuna malalamiko kuhusu malipo ya walimu tuliosimamia mitihani ya Kidato cha Pili, ambapo tumelipwa nusu ya fedha tulizostahili kulingana na makubaliano ya awali.
Tulipohoji na kufuatilia kiasi kilichobaki, tuliambiwa na uongozi kuwa hayo ndiyo malipo yaliyopangwa, licha ya kuwa mkataba wetu ulitaja kuwa tungelipwa kwa siku 10 za kazi.
Hali hii imetuacha walimu tukiwa na maswali kuhusu sababu za kulipwa kiasi hicho na kutotekelezwa kwa makubaliano yaliyofikiwa.
Tunaomba uongozi husika utoe ufafanuzi kuhusu malipo hayo na kuhakikisha kuwa walimu tunalipwa stahiki zetu kwa mujibu wa makubaliano yaliyowekwa.