Malalamiko kwa Shule Binafsi: Wizara ya Elimu na Tamisemi waliangalie na kulitolea muongozo

Watapumzika baada ya mitihani kuanzia Sept-Dec mkuu tulia dawa ipenye
Sasa mkuu kwa taarifa yako (kama haya mambo yamekupita pembeni kidogo) hakuna kitu muhimu kwenye ubongo wa binadamu yeyote kama mapumziko. Mapumziko maanake unatoka nje kidogo ya yale au utaratibu wa kila siku wa maisha uliouzoea. Ukirudi unarudi na nguvubya ajabu! Lakini watoto kuendelea na nazingira yaleyale mtihani ukifika hiyo sept. wanakuwa hoi ajili zimechoka! Matokeo yake hata performance katika mitihani inaweza kushuka!
 
Nakubaliana na Mtoa hoja..Watoto wanasona vizuri na waalimu wako vizuri kwa nini wa tunawamis Watoto wetu eti tu mna-wasupplimate wafaulu vuzuri. Serikali or rather Bunge wekeni swala hili sawa. Thanks Mzazi Ninayeumizwa na utaratibu huo.
Umelazimishwa kupeleka private na wakati kuna elimu bure? mpeleke huko akakue
 
Sasa mkuu kwa taarifa yako (kama haya mambo yamekupita pembeni kidogo) hakuna kitu muhimu kwenye ubongo wa binadamu yeyote kama mapumziko. Mapumziko maanake unatoka nje kidogo ya yale au utaratibu wa kila siku wa maisha uliouzoea. Ukirudi unarudi na nguvubya ajabu! Lakini watoto kuendelea na nazingira yaleyale mtihani ukifika hiyo sept. wanakuwa hoi ajili zimechoka! Matokeo yake hata performance katika mitihani inaweza kushuka!
Mkuu nadhani huwa wanapewa wiki moja kabla ya shule kufungua, inatosha vinginevyo watarudi na mimba bure, ndiyo maana mimba nyingi zipo government not private.
 
Tena wa chekechea ndiyo wa kuheshimu zaidi mkuu maana anaanza mtoto ambaye bado anajinyea mpaka anajitambua
Hapobupo sawa. Lakini mengine haya ya eti mtoto wa darasa la sita hafungi shule leo kwa sababu ya kujiandaa na darasa la saba mwakani hainingii akilini kabisa!

Eti lengo ni mumaliza syllabus ya darasa la saba ili watakapoingia la saba iwe ni marudio tu! Kweli? Hao waliopanga syllabus ya msingi isomwe miaka saba walipanga bila utafiti basi?
 
Ndalichako anaweza kufanya utafiti gani?
 
Suala la likizo kwa binadamu ni la muhimu.

Kilichosababisha yote haya ni udhaifu katika usimamizi wa elimu yetu. Namanisha, hapa Tanzania, matokeo mazuri ndiyo yanayozingatiwa kuliko utendaji wa kazi kwa mhitimu. Kwa maneno mengine, aliyepata division 1 ndiyo ana akili kuliko aliyepata sifuri. Kumbe hata mwenye sifuri kuna maeneo anaweza kuwa mzuri mfano michezo, ila kwa kuwa tunajali vyeti, basi inabidi tuwakaririshe (siyo kuwafundisha) watoto masomo hadi jumapili.

Hali hii imepelekea shule nyingi, (siyo za private tu, hata za serikali) msingi na sekondari kufundisha mfululizo mwaka mzima. Shule nyingine zimefikia hatua ya kutundisha hadi Disemba mada (topics) za mwaka wa darasa linalofuatia. Hali imekuwa ni mbaya sana. Watoto wanakuwa overdosed. Kuna shule moja ya sekondari, utaratibu wao ni wa kumaliza topics za form four mwezi wa tatu, wakati silabasi inataka umalize angalau August -Sept hivi.

Maafisa elimu nao hawapo nyuma kulaumiwa. Maafisa hawa hutoa vitisho kwa wakuu wa shule, ambao shule zao zitakuwa za mwisho. Wanasahau kwamba, hata wote wakipata "A", lazima apatikane wa mwisho. Matokeo yake, (sina ushahidi) inaweza kuwafanya wakuu wa shule, hasa wa shule za msingi waibe mitihani ili wasitumbuliwe. Matokeo yake, watoto wanafaulu sekondari huku mkuu wa shule akijitapa, ila watoto wengine hawajui kusoma na kuandika. Je, wataweza kusoma na kuandika Kiingereza wakiwa sekondari?

Ile dhana ya kusema elimu ni nguzo ya kumpa maarifa mwanafunzi, ili aweze kupambana na mazingira yake haipo tena kwa Tanzania. Hapa ni kuwafanya wanafunzi wafaulu mitihani. Kukaririsha watoto masomo mwaka mzima.
 
Mkuu nadhani huwa wanapewa wiki moja kabla ya shule kufungua, inatosha vinginevyo watarudi na mimba bure, ndiyo maana mimba nyingi zipo government not private.

Kama ninhivyo basi huu uwe nibutaratibu rasmi na serikali iruhusu hilo. Tuambiwe wazi kwamba huu utaratibu wa mwanzo wa wanafunzi kwenda likizo haufai kwa sababu pamoja na mengine watapata mimba! Sasa akimalisa la saba sibutakuwa naye miezi karibu mitatu na ushee? Swala la mimba ni malezi wala halihusiani moja kwa moja na kufunga na kufungua shule.
 
Fanya utafiti kwanini wanafunzi wa shule za government wanapata mimba kuliko wa private? utanipa jibu siku nyingine
 
Suala la likizo kwa binadamu ni la muhimu.

Kilichosababisha yote haya ni udhaifu katika usimamizi wa elimu yetu. Namanisha, hapa Tanzania, matokeo mazuri ndiyo yanayozingatiwa kuliko utendaji wa kazi kwa mhitimu. Kwa maneno mengine, aliyepata division 1 ndiyo ana akili kuliko aliyepata sifuri. Kumbe hata mwenye sifuri kuna maeneo anaweza kuwa mzuri mfano michezo, ila kwa kuwa tunajali vyeti, basi inabidi tuwakaririshe (siyo kuwafundisha) watoto masomo hadi jumapili.

Hali hii imepelekea shule nyingi, (siyo za private tu, hata za serikali) msingi na sekondari kufundisha mfululizo mwaka mzima. Shule nyingine zimefikia hatua ya kutundisha hadi Disemba mada (topics) za mwaka wa darasa linalofuatia. Hali imekuwa ni mbaya sana. Watoto wanakuwa overdosed. Kuna shule moja ya sekondari, utaratibu wao ni wa kumaliza topics za form four mwezi wa tatu, wakati silabasi inataka umalize angalau August -Sept hivi.

Maafisa elimu nao hawapo nyuma kulaumiwa. Maafisa hawa hutoa vitisho kwa wakuu wa shule, ambao shule zao zitakuwa za mwisho. Wanasahau kwamba, hata wote wakipata "A", lazima apatikane wa mwisho. Matokeo yake, (sina ushahidi) inaweza kuwafanya wakuu wa shule, hasa wa shule za msingi waibe mitihani ili wasitumbuliwe. Matokeo yake, watoto wanafaulu sekondari huku mkuu wa shule akijitapa, ila watoto wengine hawajui kusoma na kuandika. Je, wataweza kusoma na kuandika Kiingereza wakiwa sekondari?

Ile dhana ya kusema elimu ni nguzo ya kumpa maarifa mwanafunzi, ili aweze kupambana na mazingira yake haipo tena kwa Tanzania. Hapa ni kuwafanya wanafunzi wafaulu mitihani. Kukaririsha watoto masomo mwaka mzima.

Asante sana. Mchango murua sana! Naamini hii itasaidia katika mchakato wa kureview mfumo wetu wa elimu. Aione Mh Ndalichako!

Mchango wako huu umeweza kuonesha kwamba malalamiko yangu ni matokeo tu ya shida kubwa zaidi ya mfumo wa elimu yetu! Tumesomesha watu wataalamu wengi sana wa masuala haya elimu lakini wapo wapo ru kama hawapo huku hali ya elimu nchini ikizidi kuwa mbaya!
 
Nimekusoma: Elimu kwenye taasisi binafsi ni biashara! Hii ndio hoja yangu haswa. Hawa wafanya biashara wanapaswa wawe regulated kama biashara nyingine. Kutaka sifa kwao kusiwe kigezo cha kuwatesa watoto kwa kuwa overload. Hii nchi sio shamba la bibi kwamba yeyote anayewrza kujifanyia atakavyo bila kufuata miongozo iliyowekwa.

Nashukuru umesisitiza hapo mwishoni kwamba hawa wanavunja kanuni na raratibu za wizara!

Swala la kupeleka watoto shule za serikali kama naona private hakufai ni hoja ya ajabu kidogo. Hiki kihoja hakina tofauti na kipindi kile mtu analalamika mshahara mdogo mwendazake anajibu kama mshahara mdogo acha kazi! Is this the way to go? Kwamba huna haki ya kulalamika kwenye jambo unaloona halipo sawa? Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kubakisha watoto shuleni mwezi wa sita na ufaulu wao! Kama upo ni very insignificant! Kana upo naomba huo utafiti unaoonesha hilo!

Nimenote kwamba waalimu wengi wa private wamevamia huu uzi kuupinga kwacsababu zilizo wazi!
Hili jambo ni pana sana, kwa sheria, kazi ni masaa8, ila kama unataka upate mafaniko zaidi lazıma ufanye kazi zaidi ya hayo masaa, na Shule ni hivyo hivyo, Ukienda kwenye shule za Serikali mwanafunzi anayejituma Kusoma masaa mengi zaidi na ni wachache au wazazi wanasimamia wanafanya vizuri zaidi kwenye matokeo, kwenye dunia ya Soko huru ni lazima kuwafundisha watu kufanya kazi zaidi ili wawe bora zaidi.
 
Asante sana. Mchango murua sana! Naamini hii itasaidia katika mchakato wa kureview mfumo wetu wa elimu. Aione Mh Ndalichako!

Mchango wako huu umeweza kuonesha kwamba malalamiko yangu ni matokeo tu ya shida kubwa zaidi ya mfumo wa elimu yetu! Tumesomesha watu wataalamu wengi sana wa masuala haya elimu lakini wapo wapo ru kama hawapo huku hali ya elimu nchini ikizidi kuwa mbaya!
Hali ni mbaya sana. Wazazi na wadau wa elimu fuatilieni. Watoto wanakaririshwa masomo (hawafundishwi) kuanzia Januari mpaka Disemba, ili wafaulu mitihani. Shule zingine wanasoma Jumatatu hadi Jumapili.

Tujiulize, mbona miaka hiyo likizo zilikuwepo na wanafunzi walikuwa wanafaulu?

Tunahitaji mjadala katika mwenendo wa elimu yetu. Hali ni mbaya sana!
 
yaani watanzania sisi ni wavivu sana tena sana mfano ni huu wa watoto kuwahurumia kipindi fulani ilikuwa sheria sikukuu ikiangukia jumapili unalipizia jumatatu watu wakafurahi sana huo ni kutokuwa na ufahamu kuwa unapunguza siku za uzalishaji uchumi unarudi nyuma kwaajili tu ya kupenda kukaa nyumbani kunakusaidia nini? kwa suala la watoto kuna usemi unasema ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga ,

ukiuchukua mwaka unaweza ukauona mkubwa sana lakini ni muda mdogo sana ukianza kuugawanya ukumbuke kuna siku za sikukuu ambazo hawarudi wanakuwa shule lakini hawaingii darasani wakifungua january wanasomamapaka march wanafunga wikimbili wakifungua april hiyo hapowanasomamay tuwanafunga likizokubwa wanafungua july wanasoma september tena likizo wiki mbili wanafungu kidogo october hiyohapo november mwishoni wanafunga likizo kubwa hebu hesabu ni muda gani mwanao amesoma darasani na hesabu ni muda gani anakuwa hayuko darasani katika mwaka acheni watoto wawe busy na shule muda wanao kiaa nyumbani unatosha kabisa hata hivyo hizo likizo wanazobaki shuleni ni kwa madarasa yenye mitihani tu yaani waacheni watoto wasome KWANI HAO WANAFUNZI WENYEWE WANA SEMAJE?

kuna mzazi alishaambiwa na mtoto kuwa amechoka kusoma apumzike? tuacheni kuambukiza watoto uvivu tulionao
 
Hata baadhi ya shule za serikali darasa la nne na Saba hawafungi.
Pia wanaingia asbh saa 12 na kusoma hadi saa 11 jion.

Ni kero
 
NB: Nakala kwa: UNESCO, UNICEF, ILO, AMREF, WHO. Maana hawa jamaa wanajiona wanaishi kisiwani.
 
Ndugu yangu! Wangekuwa wanafunzi wanafundishwa hapo sawa, lakini wanakaririshwa mambo yanayohusiana na mitihani ili wafaulu. Wanawachosha tu bure.

Wangekuwa wanafunzi wanashinda shule wanafanya practicals na uvumbuzi mbalimbali hapo sawa. Lakini kunyimwa likizo kisa kukaririshwa mambo ya mitihani ni kuwachosha tu watoto na kuharibu bongo zao.
 
Hata baadhi ya shule za serikali darasa la nne na Saba hawafungi.
Pia wanaingia asbh saa 12 na kusoma hadi saa 11 jion.

Ni kero
Wanakera kweli kweli, wanasema punda afe, mzigo ufike salama kwa mwenyewe.
 
Elimu ya Tanzania kwa sasa ni ya mitihani, ieleweke hivyo. Wadau wa elimu wanalijua hilo.
 
Tunaomba serikali na hasa Wizara ya Elimu na ike ya Tamisemi waliangalie sana hili na kulitolea muongozo mapema.

Malalamiko yenyewe ni kwamba kumekuwa na utaratibu kwa shule za binafsi hasa zile za English Medium kuzuia wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwenda likizo hasa ya mwezi wa sita.

Inajulikana kwamba utaratibu wa likizo upo duniani kote kwa binadamu wote wanaofanya kazi wakiwepo wanafunzi. Na hili linafanyika baada tafiti kuonesha kwamba binadamu hawawezi kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwani hilo linaadhiri ufanisi wao katika kazi.

Sasa inashangaza kuona shule hizi za msingi za binafsi zinawanyima wanafunzi wa darasa la nne na la sita kwenda mapumziko ya mwezi mmoja eti kisa wanawaandaa kwa mitihani ijayo.

Hawa ni watoto wadogo, wanasoma mfulilizo bila kupumzika kisa mitihani kweli hili ni sawa? Kaka na dada zao wa Form Two na Form Four wana mitihani mwishoni mwa mwaka huu lakini wapo likizo. Sasa iweje hawa wa form two na darasa la sita? Ni nini hasa so special kwa hawa wanafunzi wa English Medium schools.

Je, ni kweli kwamba muda uliopo hautoshi kuwaandaa hawa watoto kufanya vizuri kwenye mitihani yao?

Hao watalaam wa elimu na wanasaikolojia waliopendekeza utaratibu huo na ukakubalika pengi walikosea?

Isitoshe, kwa sasa kuna waraka wa serikali unaokataza shule za serikali kutofunga shule au kuongeza muda wa masomo kwa wanafunzi bila ruhusa ya mkurugenzi/serikali. Tena yamewekwa masharti na mambo ya kuzingatia kama shule itataka kutumia muda wa mapumziko wa wanafunzi kufundisha.

Je, Shule hizi za private hazifungwi na taratibu na secular hizo za serikali? Wanaruhusiwa kufanya mambo wanavyoona tu wao? Kiholela.

Tunaomba serikali na bunge waliangalie hili na liwekewe utaratibu mzuri kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wazazi na kunyima haki ya watoto kupumzika "from daily routines za shule!"
Jana nimeenda shule ya msingi Shekilango, ni shule ya serikali, nimekuta kuna wanafunzi wa darasa la nne, la sita na la saba, nikauliza why hawajafunga mwalimu akanijibu tukiwaacha wakakaa nyumbani mwezi mzima wakirudi hapa July kichwani hawatakuwa na moja wanalolikumbuka thats why tumebaki nao atlleast for two weeks ndio wanende likizo
 
Kam
Tunaomba serikali na hasa Wizara ya Elimu na ike ya Tamisemi waliangalie sana hili na kulitolea muongozo mapema.

Malalamiko yenyewe ni kwamba kumekuwa na utaratibu kwa shule za binafsi hasa zile za English Medium kuzuia wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwenda likizo hasa ya mwezi wa sita.

Inajulikana kwamba utaratibu wa likizo upo duniani kote kwa binadamu wote wanaofanya kazi wakiwepo wanafunzi. Na hili linafanyika baada tafiti kuonesha kwamba binadamu hawawezi kufanya kazi mfululizo bila kupumzika kwani hilo linaadhiri ufanisi wao katika kazi.

Sasa inashangaza kuona shule hizi za msingi za binafsi zinawanyima wanafunzi wa darasa la nne na la sita kwenda mapumziko ya mwezi mmoja eti kisa wanawaandaa kwa mitihani ijayo.

Hawa ni watoto wadogo, wanasoma mfulilizo bila kupumzika kisa mitihani kweli hili ni sawa? Kaka na dada zao wa Form Two na Form Four wana mitihani mwishoni mwa mwaka huu lakini wapo likizo. Sasa iweje hawa wa form two na darasa la sita? Ni nini hasa so special kwa hawa wanafunzi wa English Medium schools.

Je, ni kweli kwamba muda uliopo hautoshi kuwaandaa hawa watoto kufanya vizuri kwenye mitihani yao?

Hao watalaam wa elimu na wanasaikolojia waliopendekeza utaratibu huo na ukakubalika pengi walikosea?

Isitoshe, kwa sasa kuna waraka wa serikali unaokataza shule za serikali kutofunga shule au kuongeza muda wa masomo kwa wanafunzi bila ruhusa ya mkurugenzi/serikali. Tena yamewekwa masharti na mambo ya kuzingatia kama shule itataka kutumia muda wa mapumziko wa wanafunzi kufundisha.

Je, Shule hizi za private hazifungwi na taratibu na secular hizo za serikali? Wanaruhusiwa kufanya mambo wanavyoona tu wao? Kiholela.

Tunaomba serikali na bunge waliangalie hili na liwekewe utaratibu mzuri kwa sababu linaleta usumbufu mkubwa kwa wazazi na kunyima haki ya watoto kupumzika "from daily routines za shule!"
Kama ni mwathirika wa hilo chukua hatua unayoona inafaa, ikiwa ni pamoja na kuukata huo utaratibu, vipi kama wazazi wengine wanaukubali, yawezekana hawana muda wakuwalea watoto wao hivyo wanaona bora waendelee kuwa mikononi mwa walimu wao.
 
Mwandiko wako tu, unatoa picha halisi ya watu wanaofanya kazi mfululizo bila kuheshimu muda wa mapumziko. Hawafuati kanuni za uandishi. Hawazingatii mahali sahii pakuweka, vituo, mikato, herufi kubwa, na kadhalika. Ukisha poteza umakini katika mambo ya msingi basi hata ukikesha unakesha bure. Hakuna kazi hapo, wala ufanisi h'utouona!
 
Back
Top Bottom