Suala la likizo kwa binadamu ni la muhimu.
Kilichosababisha yote haya ni udhaifu katika usimamizi wa elimu yetu. Namanisha, hapa Tanzania, matokeo mazuri ndiyo yanayozingatiwa kuliko utendaji wa kazi kwa mhitimu. Kwa maneno mengine, aliyepata division 1 ndiyo ana akili kuliko aliyepata sifuri. Kumbe hata mwenye sifuri kuna maeneo anaweza kuwa mzuri mfano michezo, ila kwa kuwa tunajali vyeti, basi inabidi tuwakaririshe (siyo kuwafundisha) watoto masomo hadi jumapili.
Hali hii imepelekea shule nyingi, (siyo za private tu, hata za serikali) msingi na sekondari kufundisha mfululizo mwaka mzima. Shule nyingine zimefikia hatua ya kutundisha hadi Disemba mada (topics) za mwaka wa darasa linalofuatia. Hali imekuwa ni mbaya sana. Watoto wanakuwa overdosed. Kuna shule moja ya sekondari, utaratibu wao ni wa kumaliza topics za form four mwezi wa tatu, wakati silabasi inataka umalize angalau August -Sept hivi.
Maafisa elimu nao hawapo nyuma kulaumiwa. Maafisa hawa hutoa vitisho kwa wakuu wa shule, ambao shule zao zitakuwa za mwisho. Wanasahau kwamba, hata wote wakipata "A", lazima apatikane wa mwisho. Matokeo yake, (sina ushahidi) inaweza kuwafanya wakuu wa shule, hasa wa shule za msingi waibe mitihani ili wasitumbuliwe. Matokeo yake, watoto wanafaulu sekondari huku mkuu wa shule akijitapa, ila watoto wengine hawajui kusoma na kuandika. Je, wataweza kusoma na kuandika Kiingereza wakiwa sekondari?
Ile dhana ya kusema elimu ni nguzo ya kumpa maarifa mwanafunzi, ili aweze kupambana na mazingira yake haipo tena kwa Tanzania. Hapa ni kuwafanya wanafunzi wafaulu mitihani. Kukaririsha watoto masomo mwaka mzima.