Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

Nina kawaida ya kuweka vifurushi vya simu kila wiki. Leo naingia kwenye mtandao wa Tigo nakutana na mabadiliko ya ajabu ya bei za vifurushi.

Nikaamua niangalie na Voda nako kukoje? Balaa ni lile lile hakuna nafuu, nikajiuliza kulikoni mabadiliko ya ghafla hivi ya bei za vifurushi kama soko la Tandale?

Baada ya tafakari nikagundua kuwa kampuni za simu zimechukulia nafasi hii ya TCRA kushikamana na NIDA kama nafasi ya kujipigia pesa kukiwa na taharuki.

TCRA imejionyesha nayo ni taasisi dhaifu sana katika usimamizi, jee nani hasa kiongozi wa kisiasa anayepaswa kulisimamia hili? Ni Mwakyembe au nani?

TCRA imeshindwa mitandao ya simu na kampuni za ving'amuzi sijui kwa nini, hadi inadhaniwa kuwa wakuu wake wameingizwa kwenye payrolls za makampuni hayo yanayofanya biashara kimafia.
 
Sio 1,000(elfu moja ) ni Tsh 10,000.(elfu 10)



IMG_8558.JPG
 
Halotel
1,000 = GB1 + Dakika 10 (siku 7)
5,000 = GB7 (siku 7)
10,000 = GB 10 (siku 30)

HaloPesa Mega bando.
*150*88#
Chagua vocha na vifurushi
Chagua MEGA bando


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom