Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Hawa jamaa wanafanyaga meeting wanaitana mitandao yote halafu wanakubaliana namna ya kuuza vifurushi vyao ili kusudi kuepukana na kadhia ya kukimbiwa na wateja wao endapo upande wa pili kutakuwa na gharama za chini kwenye vifurushi.Ndio maana Voda niliwakimbia kitambo sana.
Mfano: Kama Halotel ni mtandao ambao ni mpya bado haujawa popular sana kama hiyo mingine ambayo ina miaka si chini ya saba. Kwaiyo unakuta kwasababu ni mgeni hivyo amepewa unafuu kwenye mabando yake kwani naye akiweka bei juu vifurushi vyake mtandao wake hautakuwa na users wengi ukizingatia na sisi Wabongo tunavyopenda kitonga.
Halotel kwenye laini yao ya chuo walikuja na bundle la wiki MB 600 kwa shingi 500 halafu unapewa na speed ya maana ili kukamata watu. Kama kawaida watu walivyojaa kwa kiwango walichokua wanakitaka wakaanza kupunguza MB100 ikawa kwa jero unapata MB500.
Watu tukaona fresh tu kwa speed ya halotel zinatutosha, tumeenda baada ya muda tena wakaanza kutuwekea vitengo, mara ukinunua MB za jero unapata MB500 ila sharti la hizo MB's ni kwamba katika MB150 lazima uzitumie ku-stream youtube kinyume na hapo utajikuta umetumia MB350.
Saizi wamezipunguza tena zimekuwa MB250, sasa kwa kukimbilia hakupo.