Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

Ndio maana Voda niliwakimbia kitambo sana.
Hawa jamaa wanafanyaga meeting wanaitana mitandao yote halafu wanakubaliana namna ya kuuza vifurushi vyao ili kusudi kuepukana na kadhia ya kukimbiwa na wateja wao endapo upande wa pili kutakuwa na gharama za chini kwenye vifurushi.

Mfano: Kama Halotel ni mtandao ambao ni mpya bado haujawa popular sana kama hiyo mingine ambayo ina miaka si chini ya saba. Kwaiyo unakuta kwasababu ni mgeni hivyo amepewa unafuu kwenye mabando yake kwani naye akiweka bei juu vifurushi vyake mtandao wake hautakuwa na users wengi ukizingatia na sisi Wabongo tunavyopenda kitonga.

Halotel kwenye laini yao ya chuo walikuja na bundle la wiki MB 600 kwa shingi 500 halafu unapewa na speed ya maana ili kukamata watu. Kama kawaida watu walivyojaa kwa kiwango walichokua wanakitaka wakaanza kupunguza MB100 ikawa kwa jero unapata MB500.

Watu tukaona fresh tu kwa speed ya halotel zinatutosha, tumeenda baada ya muda tena wakaanza kutuwekea vitengo, mara ukinunua MB za jero unapata MB500 ila sharti la hizo MB's ni kwamba katika MB150 lazima uzitumie ku-stream youtube kinyume na hapo utajikuta umetumia MB350.

Saizi wamezipunguza tena zimekuwa MB250, sasa kwa kukimbilia hakupo.
 
Yes nakula 1GB kwa 10 days kwa 1000. *149*01# >>> 2 >>> 2
Ukitaka kuona upuuzi wa hawa Tigo endelea kufululiza kununua hicho kifurushi kama hawakitoa basi utakinunua kwa Sh.3500

Mimi laini yangu ya Tigo sikuwahi kuiwekea vocha ndani ya miezi mitatu basi wakaanza kunitamanisha na offer zao kua weka jero upate MB500 kwa siku tatu. Mi nikawa nawapuuza kwasababu kipindi hicho Halotel nilikua napewa MB 600 kwa jero.

Siku moja nikastuka kuona meseji kwenye laini yangu ya Tigo kua ukiweka vocha ya 500 utapewa GB 30 zakutumia mwezi mzima. Nikasema acha nijaribu kama watanitapeli jero siyo kesi kwasababu siyo hela kubwa.

Nilivyoweka nikajiunga ikakubali aisee nilifurahi sana nikawapiga chini halotel kwa muda nikawa na download vitu heavy torrentz ikawa shangwe sana

Lakini baada ya mfululizo wa siku tatu kuunga bando hilo nikishangaa sana ile menu niliyokua napata lile bando ikageuzwa kua menu ya kukopea

Mi sina hili wala lile nimeweka jero langu nataka nijiunge nakuta hongera umefanikisha kukopa sh 600, aaah nilimaindi kisenge
 
Scars,
Kwa sasa nimekimbilia Airtel. Japokuwa internet yao bado ipo udoro udoro lakini hivyo hivyo tunasogeza siku.

Japokuwa nao wameleta ujinga mmoja. Eti kifurushi cha 500, unapata Dk 40 (Airtel-Airtel), Dk 20 (Mitandao yote), SMS 500 na MB 500. Hizo MB 500 ni sharti utumie MB 250 mchana na hizo nyengine usiku kuanzia saa 6.
 
Tangu tigo wapandishe bei ya vifurushi nimehamia HALOTEL
Maana wameona maisha wameyapatia VODA wao nina mwaka wa pili labda kufanya miamala na m-pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
Halotel nao wadwanzi kubabake zao

Kifurushi cha kupitia halopesa kilikua kina dakika 100 na GB1 saizi wamefyeka dakika 90 wametuachia 10

Kama hiyo haitoshi kuna ile night pack ya ofa tulikua tunaipata kwa buku halafu unlimited tena yenye kasi kubwa, saizi imekua buku jero halafu kuanzia saa sita lina speed ya JB, mpaka saa tisa na nusu hivi ndo utaona speed ya Usain Bolt.
 
Kwa sasa nimekimbilia Airtel. Japokuwa internet yao bado ipo udoro udoro lakini hivyo hivyo tunasogeza siku.

Japokuwa nao wameleta ujinga mmoja. Eti kifurushi cha 500, unapata Dk 40 (Airtel-Airtel), Dk 20 (Mitandao yote), SMS 500 na MB 500. Hizo MB 500 ni sharti utumie MB 250 mchana na hizo nyengine usiku kuanzia saa 6.

...
Huku Airtel network yao inasumbua, kila muda ni emergency call tu.
 
Halo na TTC L speed mbovu mkuu
Kwa sa hivi kama hutumii TTCL au Halotel unawakati mgumu sana wa bando. Tena nao hadi ujue vifurushi vyao vizuri vilipo kama Halotel wamevificha vifurushi vyao kwenye Hallopesa... Tigo acha ibaki kwa Tigo pesa tuu... Kwakweli Tigoni keromtu najiunga unanipa msg 5? sasa zinakaI gani .. Et mia 5 unapata dakika 7 mitandao yote sijui na vimeseji vingapi.. Wakati halloteli wanakupa 18

Maisha ni kupanga na kuchagua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Airtel nawakubali sana
IMG_20200126_010952_977.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa nimekimbilia Airtel. Japokuwa internet yao bado ipo udoro udoro lakini hivyo hivyo tunasogeza siku.

Japokuwa nao wameleta ujinga mmoja. Eti kifurushi cha 500, unapata Dk 40 (Airtel-Airtel), Dk 20 (Mitandao yote), SMS 500 na MB 500. Hizo MB 500 ni sharti utumie MB 250 mchana na hizo nyengine usiku kuanzia saa 6.

...
Hicho kifurushi kuna muda ikifika watakimega, kama mm tu walivyonifanyia.
 
Back
Top Bottom