Nina kawaida ya kuweka vifurushi vya simu kila wiki. Leo naingia kwenye mtandao wa Tigo nakutana na mabadiliko ya ajabu ya bei za vifurushi.
Nikaamua niangalie na Voda nako kukoje? Balaa ni lile lile hakuna nafuu, nikajiuliza kulikoni mabadiliko ya ghafla hivi ya bei za vifurushi kama soko la Tandale?
Baada ya tafakari nikagundua kuwa kampuni za simu zimechukulia nafasi hii ya TCRA kushikamana na NIDA kama nafasi ya kujipigia pesa kukiwa na taharuki.
TCRA imejionyesha nayo ni taasisi dhaifu sana katika usimamizi, jee nani hasa kiongozi wa kisiasa anayepaswa kulisimamia hili? Ni Mwakyembe au nani?
TCRA imeshindwa mitandao ya simu na kampuni za ving'amuzi sijui kwa nini, hadi inadhaniwa kuwa wakuu wake wameingizwa kwenye payrolls za makampuni hayo yanayofanya biashara kimafia.