Sisi vijana tulioajiriwa kuwa Maafisa Kilimo wa zao la pamba kupitia programu ya BBT, tunakabiliwa na changamoto ya kucheleweshewa mishahara na stahiki nyingine zinazohusiana na utekelezaji wa majukumu yetu.
Baada ya kuajiriwa na Bodi ya Pamba na kupangiwa kufanya kazi katika kampuni mbalimbali, tumekuwa tukikumbana na ucheleweshaji wa mishahara. Wakati mwingine tunakaa hadi miezi miwili au mitatu bila kulipwa.
Aidha, tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya kucheleweshewa fedha za mafuta kwa ajili ya pikipiki tunazotumia kutekeleza majukumu yetu. Hali hii inafanya iwe vigumu kwetu kutekeleza majukumu kwa ufanisi, licha ya kuwa tunatarajiwa kuwahudumia wakulima na kutimiza malengo ya programu.
Tunaomba Wizara ya Kilimo iingilie kati suala hili na kuhakikisha mishahara pamoja na stahiki zetu zinalipwa kwa wakati, ili tuweze kutekeleza majukumu yetu ipasavyo bila kukumbana na changamoto za kifedha.
Tunaomba suala hili lishughulikiwe kwa haraka kwa maslahi ya vijana, wakulima na mafanikio ya programu ya BBT.