KERO Malalamiko ya kukosekana kwa Dawa za Saratani (Chemotherapy) kwa bima ya NHIF, Muhimbili Mloganzila

KERO Malalamiko ya kukosekana kwa Dawa za Saratani (Chemotherapy) kwa bima ya NHIF, Muhimbili Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mgonjwa wangu anasumbuliwa na tatizo la Saratani na kwa sasa yupo kwenye mzunguko wa matibabu ya Kemotherapy (Chemotherapy), Hospitali ya Taifa MUHIMBILI (MLOGANZILA).

Hivi karibuni tumeelezwa na wataalamu kuwa Dawa za Chemotherapy anazotakiwa kupata mgonjwa wangu hazipo/zimeisha hospitalini hapo, na tumeelekezwa kuwa kama tuna uwezo wa kifedha, tununue wenyewe au tulipie kwa fedha taslimu (Cash).

Jambo hili limetuletea hofu na mzigo mkubwa sana kwa sababu zifuatazo: Mgonjwa wangu anatumia Kadi ya Bima ya Afya ya NHIF ambayo iko hai na inagharamia huduma za matibabu ya saratani kisheria na kikanuni.

Dawa hizi za saratani ni za gharama kubwa sana ambazo mwananchi wa kawaida hawezi kuzimudu kwa fedha za mfukoni, na ndiyo maana tunategemea mfumo wa Bima ya Afya.

Kukatika au kuchelewa kwa ratiba ya Dawa za Chemotherapy kunaweka maisha ya mgonjwa wangu hatarini na kunaweza kurudisha nyuma maendeleo ya afya aliyotakiwa kuyapata.

Je, utaratibu wa sasa wa NHIF na Hospitali ya Taifa Muhimbili unazitaka familia kujigharamia dawa hizi pindi zinapokosekana hospitalini, au kuna utaratibu maalum wa mgonjwa wa bima kupatiwa dawa kutoka maduka ya nje (panel/authorized pharmacies) kupitia bima yake?

Mipango gani ya dharura ipo ili kuhakikisha wagonjwa wa saratani wanaotegemea NHIF hawakati mikataba yao ya matibabu pale dawa zinapokosekana kwenye bohari ya hospitali?

Tunasaidiwaje kwa haraka ili wagonjwa wapate dawa hizi kwa wakati na kuokoa maisha yao?

Hii cash siyo kwamba wananunua dawa ndani ya Mloganzila hata wao wanasema wananunua maduka ya nje, maana katika hela unayolipa unaongeza 10,000 ya bodaboda. Kuna Muhusika pale, ndiyo unampa hiyo hela ya dawa na hiyo ya boda, nayeye anasema anaagiza.
 
Dawa zipo, inategemea umejiunga na kifurushi kipi na pia endapo ushatuma maombi ya huduma husika

Changamoto ni kwa Bima ya Afya kwa wote ...... Je matibabu hayo yanapatikana?
 
Back
Top Bottom