Malalamiko ya mbunge wa Mbogwe yasipuuzwe. Anadai wanalipwa mil 3.8. Hataki kufanya ujanja ujanja kama wabunge wengine. Ni ujanja gani?

Malalamiko ya mbunge wa Mbogwe yasipuuzwe. Anadai wanalipwa mil 3.8. Hataki kufanya ujanja ujanja kama wabunge wengine. Ni ujanja gani?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Mbunge wa Jimbo la Mbogwe ameendelea kukazia zege kauli yake aliyoitoa bungeni juu ya maslahi ya wabunge.

Anadai yeye ni msema kweli daima, ameokoka na hataki kufanya yasiyopendeza Mungu.

Amefunguka kwa kusema kuwa wabunge wanalipwa milioni 3.8 tu. Ambazo kimsingi hazitoshi kwa kazi anayoidanya mbunge.

Anasema yeye hataki kufanya ujanja ujanja kama wabunge wengine. Hapa ndipo kuna swali la msingi. Ni ujanja gani huo unaofanywa na wabunge wengine ambao mbunge huyu mcha Mungu hataki kuufanya ili kujiongezea kipato?

Ni wezi?
Wala rushwa?
Wanaiibia serikali kwa mlango wa nyuma?

Natamani wanahabari muendelee kumhoji huyu mbunge Maganga, mbunge wa Mbogwe ili atujuze. Au kama kuna mwenye kujua zaidi atuambie.

Screenshot_20210623-165906.png
 
Kupokea rushwa kwenye kamati zao. Wewe unafikiri kwanini wanapenda kamati ya madini
 
Wabunge wajanja sana, waliweka mshahara mdogo kwa maksudi ili wakwepe kodi, wakati huo huo wakajiwekea posho or allowances kibao, mbunge ana allowances zaidi ya 15 mil.. Hii yote ni kukwepa kodi. Basi wageuze mshahara mil 15 na allowances mil 3.8, labda huyu mbunge hakujua sbb gani wenzao waliweka huo mshahara mdogo kwa makusudi maalum.
 
Hata 3.8 kwa yale wanayofanya bungeni naona hawastahili hata laki 3 kwa mwezi ingewatosha.

Kwani wana kazi gani hasa ambayo wasipoifanya nchi itaathirika? Kipi wanachofanya hasa? Kupiga meza?? Kujipendekeza kwa Rais ili wapate uwaziri?
 
Wanahabari wanaweza kuwahoji wabunge wengine pia kuhusu huo ujanja ujanja ?
 
Kwa mfumo wetu wa kijani mambo yetu huwa tunaongelea chumbani.
Huyu Mbunge Mangula anapitia faili lake.
 
Huyu ni mbunge wa nchi gani ?
Hiyo milioni 11 alilipwa kwa ajili ya nini ?👇
 
Hawa wabunge wa Ccm hata hiyo 3.8M anayodai wanalipwa ni kubwa sana! Asijifananishe na wabunge wa Kenya na Nigeria ambao wanawatumikia vilivyo wananchi wao!
 
Je amefanya kazi gani? Ubunge huu huu walipopewa bure? Wanakaa na kusinzia huku wamejiwekea posho mlima, na mshahara kishuguu ili kuwalaghai maskini.
 
Alafu wanawaambia watu kitaa wajiajiri wenyewe ?

Wangeanza kuonyesha mfano akitoka bungeni aingie mtaani afanye mishe mishe za hapa na pale Tena yeye ana gari kabisa anaweza kuweka bidhaa zake za umachinga kwenye buti tofauti na watambea kwa miguu...
 
Wanafuatwa na wananchi kuombwa pesa, siyo ama ndugu zao? Sasa mfuko wa jimbo wanafanyia nini, si uliwekwa kwa sababu hizo hizo,kipindi kile cha jasusi mbobezi?
 
Achape lapa ana kipi cha zaidi amechnagia bungeni, kama anaona hela haitoshi ajiuzulu maana ni haki yake pia!
 
Huyo mbunge wa mbogwe aseme kwanza kabla ya ubunge huko alikotoka alikuwa analipwa shs ngapi mpaka aone hizo ndogo ? .
 
Aelezee huo ujanja ujanja....mpaka sasa kashiriki huo ujanja ujanja
 
Back
Top Bottom