DOKEZO Malalamiko ya watalii Arusha Airport wizara husika iamke usingizini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hujaelewa mkuu ni mita 3 hadi 5.
Najua unafahamu kuwa airpot taxi inakushusha umbali mfupi kuingia departure na eneo la ukaguzi
Nenda ata mbezi au stendi yoyote ya mabasi... alafu achukue mzigo wako kutoka ktk basi mpaka eneo la ukaguzi /getini uone kama hato kudai

Au boda uende nae umbali mfupi uone nini kitatokea
 
mkuu umeongea mengi sana shukran kwa kutujuza lakini unafahamu kwamba airport sio sehemu sawa na stendi ya mabasi yaendayo mikoani?haimake sense kwamba unaweka utaratibu airport kama ule utaratibu wa stendi ya mabasi ya kwenda mikoani(kuruhusu kikundi cha watu kufanya kazi isiyo rasmi bila makubaliano na mteja)kama kulikuwa na ulazima(dharura) huyo meneja wa uwanja angetafuta utaratibu mwingine wa kistaarabu kuepusha kero kwa wateja...tatizo sio gharama zinazotozwa bali hakuna kero kama kudaiwa pesa za malipo kwa huduma ambayo hamjakubaliana au hamjafahamishwa kabla ya kuoewa huduma
 
Hii ndio Tanzania aliyoinajisi Jiwe.
Trafiki ruksa kuchukua pesa licha ya kupata mshahara, na posho laki 4 .
Unashangaa pota kudai fedha aliyoifanyia kazi?
 
hii nchi watu wana tamaa za kipuuzi mpaka aibu kabisa, maeneo yote ya utalii utakutana na wahuni kama hao. Ni Aibu kabisa.
 
Labda tukuulize mchangiaji.
1. Uwanja umeanza kukarabatiwa lini? Na kile kikundi Kiko hapo tangu lini?

2. Walalamikaji kwenye account ya Arusha Airport mtandaoni ni wazawa au ni wageni?
Isije ikawa unajitahidi kuijibu hoja Kumbe uko nje ya mada. Karibu.
 
Tujibu. Kikundi kilianzishwa lini! Na ukarabati wa Airport ulianza lini?

Na walalamikaji kwenye account ya Arusha Airport mtandaoni ni wazawa au ni watalii?

Tuanzie hapo
 
Si jambo la kushangaza kabisa nowdayz viwanja vingi security officers wanakosea sana unakuta mda wa ndege kuondoka wao ndio wanajifanya wasaidizi wa mizigo ya abiria wanaingia mpka airside ( Rushwa mbili ya ngono na pesa) inaombwa kibabe kabisa hapa
 
Si jambo la kushangaza kabisa nowdayz viwanja vingi security officers wanakosea sana unakuta mda wa ndege kuondoka wao ndio wanajifanya wasaidizi wa mizigo ya abiria wanaingia mpka airside ( Rushwa mbili ya ngono na pesa) inaombwa kibabe kabisa hapa
 
Ndugu tueleze kile kikosi kazi kilianzishwa lini?
Wewe umesema kilianzishwa kipindi Cha ukarabati wa Airport Kitu ambacho si kweli.

Arusha Airport imeanza ukarabati huo wa Majengo kipindi cha Magu. Tena kukatokea kashfa ya matumizi mabaya ya pesa. Waziri mkuu akaenda hapo Ndio wakajifanya bado walikuwa hawajakamilisha kwa hiyo pesa bado zipo
Wakazitapika hao waliokuwa wamezichimbia. Tuliache hilo kwanza sio target yetu kwa leo.

Kwa kukusaidia kile kikundi kiko pale almost miaka 11 sasa. Tangu Mama Dede akiwa Manager wa uwanja uache kupotosha umma
Wakibeba mabegi. Wakipewa zile dollar kuna Boss wao ambaye ndie kafara na Founder wa hicho kikundi anapelekewa zile dollar vile zilivyo kama hesabu yake ya siku. Na zile zilizozidi kama faida yao anazinunua hadi sasa dollar's zote lazima wampelekee wao.

Mwisho. Ukijibu hoja jipange kuna wanaojua mambo kuliko wewe kama umetumwa kumsafisha mtu Mwambie umechafuka sana unanuka.

Ingia account ya Google Arusha Airport soma complainers almost wote ni wazungu
Je Utasema wazungu wanawachukia? Wanawajua? Wenzetu wazungu wanafikiri mbele zaidi na katika uwazi Kwamba ukikosolewa unajirekebisa ndio biashara zinavyofanyika
Na lazima upitie Kila malalamiko ya Mgeni uyajibu. Cha kusikitisha hakuna hata mmoja yuko responsible kujibu wageni wanacholalamikia
Alafu linakuja kutujibu sisi huku hata aibu halina.
Rudi shule ukajifunze kufanya biashara na watalii
Biashara ikilalamikiwa unajitokeza unajibu. Ili wateja wengine wakitaka kuandika kitu hicho hicho waone kimeshajibiwa waache kuandika

Sasa nyie mnakaa kimya mnakuja kutujibu sisi kisa mmeona Siri imefichuka. Ni tumeona tuwasaidie wageni kufikisha ujumbe
Airport ni biashara inahitaji viongozi wanaojua biashara na costomer cares

Jamani Basila wewe! Jiheshimu basi
 
Arusha tumezidi kuwa ombaomba aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…