Malalamiko yangu kwa mitandao ya simu, hasa Halotel na Voda!

Malalamiko yangu kwa mitandao ya simu, hasa Halotel na Voda!

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Baadhi ya mitandao (kama sio yote) imekuwa na utaratibu wa kukata pesa kwenye salio la muda wa maongezi pasipo sababu.

Yaani mtu hujajiunga na huduma yoyote lakini unashangaa salio limekatwa.

Hivi wakikata hizo mia mia au mia mbili kwa watu laki 1 si wanapata faida sana? Kwanini wanafanya hivyo? Haya makampuni ya simu yaache wizi. Isitoshe vifirushi viko juu, ni vile tu hakuna namna nyingine! Sijapenda.

Halafu mbaya zaidi ukipiga huduma kwa wateja, simu haipokelewi! Duh!
 
Nimejibizana na Voda kupitia Twitter(DM) hadi nimenyoosha mikono. Hawatatui tatizo, eti kila mara nisubiri niunganishwe na muhusika utadhani yupo Pluto.

Wanakiburi mno sijui kisa wana wateja wengi. Tuumie tu hivi hivi hatuna pa kwenda kulalamika. Mamlaka husika zipo mifukoni mwao.
 
halotel ndo wamezidi

ukijiunga kifurushi wanakwambia bonyeza moja ili usikatwe salio la kawaida lkn cha ajabu hata ukifanya hvyo bado wanakata

hallotel kwa kweli sijapenda hii tabia
 
Wapigie

Uwaambie wakome kukata pesa zako.
Pia wakutoe huduma zote walizokuunga au ulizojiunga kwa kujua na kutokujua.

Tena jiunge na huduma ya kusitisha matumizi bila bando. Ni kwamba kama uko na salio kwa simu halitumiki mpaka ujiunge na bando.

Mwisho waambie wakome kukutumia na sms zao za promotion.

Ukikatwa tena cheki your siblings

Case closed.
 
Baadhi ya mitandao (kama sio yote) imekuwa na utaratibu wa kukata pesa kwenye salio la muda wa maongezi pasipo sababu...
Kulikuwa na tatizo tigo, ilikuwa unaweka muda wa maongezi, mfano 2000, unajiunga voice call package ya 1000, ukipiga simu inakula kwenye 1000 iliyobaki mpaka iishe ndipo ianze kule ulikojiunga
 
Baadhi ya mitandao (kama sio yote) imekuwa na utaratibu wa kukata pesa kwenye salio la muda wa maongezi pasipo sababu...
Tumeshaambiwa kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba zake Sasa unafikiri sisi akina mitandao ni bata..??
Vimia vyenu tu mmenuna mnakuja na mabango makubwa mnatuita wezi!,sisi tule wapi..?
Kodi tutolee wapi?

Kwanza wengine msilalamike tunawafichia siri nyingi tu mbona mnamichepuko mingi hivyo hatusemi kwa watu wenu.

Mnatukanana mkiongea hatuwasemi tisiaraei!! Hamna shukurani nyinyi
 
halotel ndo wamezidi

ukijiunga kifurushi wanakwambia bonyeza moja ili usikatwe salio la kawaida lkn cha ajabu hata ukifanya hvyo bado wanakata

hallotel kwa kweli sijapenda hii tabia
Yaan...hii mitandao inafanya inavyoona wao inafaa. Ni kama hawana sheria wala utaratibu.
Wanalazimisha wateja wao kujiunga na huduma wasizotaka
 
Baadhi ya mitandao (kama sio yote) imekuwa na utaratibu wa kukata pesa kwenye salio la muda wa maongezi pasipo sababu...
Kuna siku nimewapigia voda kwanini wamekata hela wakati sijajiunga na huduma zao,baada ya kukosa majibu ya kuniridhisha wakasema niingiye ktk menyu niangaliye matumizi.Nikawauliza kama wao ktk mitambo yao hawajaona huduma nilizojiunga hiyo menyu itasaidia nini.

Halafu cjuwi wameajiri watu wengine wasiyo na weledi unakuta ktk jambo moja huyu anasema vile huyu hivi.Na halotel juzi nimeweka buku wamekata 250nikashindwa kujiunga kifurushi pendwa.

Nyie mitandao jirekebisheni tutahamasishana tuwahame.
 
Baadhi ya mitandao (kama sio yote) imekuwa na utaratibu wa kukata pesa kwenye salio la muda wa maongezi pasipo sababu...
Kampuni za simu za Tanzania ni za hovyo sana. TIGO nao ni matapeli pia wa pesa za wateja wao.

Yaani sijui Tanzania tuna mkosi gani na TCRA wapo.
 
Ahaa, basi ni tabia yao.
Ni uonevu! Kama wana hali mbaya waombe kuchangiwa kwa hiari. Na sio kukata bila taarifa. Huo ni wizi!
Kuna siku nimewapigia voda kwanini wamekata hela wakati sijajiunga na huduma zao,baada ya kukosa majibu ya kuniridhisha wakasema niingiye ktk menyu niangaliye matumizi.Nikawauliza kama wao ktk mitambo yao hawajaona huduma nilizojiunga hiyo menyu itasaidia nini.Halafu cjuwi wameajiri watu wengine wasiyo na weledi unakuta ktk jambo moja huyu anasema vile huyu hivi.Na halotel juzi nimeweka buku wamekata 250nikashindwa kujiunga kifurushi pendwa.Nyie mitandao jirekebisheni tutahamasishana tuwahame.
 
Hiik tabia ndio imefanya salio la akaunti kuu kwenye laini liwe TShs. 0. Siweki salio la kawaida hata mara moja.

Kuna siku jamaa yangu alinitumia 500 ya vocha ya kawaida badala ya tigopesa. Lile salio lilikuwa linaliwa mia mia , sasa wakanitumia meseji kuwa nimejiunga promotion gani sijui na wamekata 200 au 300 hivi.

Niliwapigia simu customer care wao niliwatukana hawatakaa wasahau. Na nikawaambia sitaki ujinga wao na waniondoe kwenye upumbavu wao. Jamaa wa pembeni hawakuamini kuwa nikichukia naweza kusema mbovu namna ile.

Dakika chache tu meseji kibaozimeingia kwenye simu kuwa nimejitoa kwenye mahuduma yao ya kijinga . Waliniambia nijitoe kwenye huduma hizo, nikawaambia kwa kuwa wao ndio wameniunganisha wao ndio waniondoe ,tena wasinisumbue kabisa.
 
Back
Top Bottom