Malaria yapata Chanjo na WHO imeithibisha, utafiti ulianza mwaka 1980

Malaria yapata Chanjo na WHO imeithibisha, utafiti ulianza mwaka 1980

Kama utafiti wa chanjo ya malaria ulianza 1980 hii covid vipi tena, maana utafiti umefanyika na chanjo kupatikana ndani ya mwaka mmoja....
 
Ziletwe tu. Maana malaria ni katili kwa watoto na mama wajawazito.
Juzi tulipoteza mama mjamzito na kichanga chake tumboni sababu ya malaria, alipimwa na kukutwa na malaria ila kibaya zaidi na figo zake zikafail muda mfupi baadae.
Pumzika kwa amani mama na mtoto!
Magonjwa yasiyowaguza mabeberu huwa sio ajenda kubwa!
 
utasikia mabeberu wanataka kutuua hawa na haya machanjo yao..
Mkuu nikupe zoezi dogo, nenda kituo chochote wanachotoa chanjo ya covid-19 waombe kwa upole wakupe ile karatasi ya maelezo ya chanjo ambayo kila dawa yoyote ya binadamu hata Aspirin huwa nayo.
Ile karatasi yenye maelekezo kwa lugha zote kuu duniani, Ike karatasi ambayo inakueleza ni yupi anastahili na yupi hastahili kupata dawa/chanjo husika, ni karatasi inayokuonyesha madhara madogo na makubwa yatokanayo na matumizi ya dawa/chanjo husika....nk.
Mkuu kwenye chanjo tunayochoma wabongo likaratasi ni jeupe pe! Hawakuandika kitu....yaani mzungu alichoka kuandika akaweka plain paper ili Mama Gwajima na TMDA wajaze wenyewe!
 
Back
Top Bottom