Malawi wameweza, Tanzania tunafuatia

Usifananishe Tanzania na vitu vya hovyo

Unajua kuwa Ccm ndio chama bora zaidi Africa ! na cha pili duniani kwa ubora !
Soma [emoji121] upinzani wa Tanzania kama ni mtoto hata kutambaa hajaanza
Ni kweli. Malawi wana independent judiaciary, jeshi neutral na wananchi wanaojielewa. Matokeo yanaruhusiwa kupingwa mahakamani. Kwa kweli Malawi kuna demokrasia kubwa sana. Hiyo ni tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania.
 
Kwa ushauri wako tufanyeje? Kama mnaona hatuwezi basi badilisheni sheria turudi kwenye mfumo wa chama kimoja.
Hakuna haja ya sheria hio kwa sababu it's officially tumesharudi kwny mfumo huo,au wewe bado haujaona?

Nakwambia tena tuache kujilisha upepo kwa tume hii ushindi kwa upinzani ni IMPOSSIBLE.

Tegemea kukuona hapa jukwaani Nov. Ukipiga kelele za kuchakachuliwa.
 
Mipango Bora ndio kila kitu,
Hapa kwetu sioni Chama Wala watu wa Aina hiyo Kwa sasa
 
Umeangalia sifa za huyo mgombea? Siyo DJ, Siyo mwanaharakati. Unatumia vigezo duni ili upate matokeo kama ya Malawi?
 
Wa kulaumiwa ni Nyerere ndie aliyetuletea hii mifumo mibovu ya uongozi,Kama mtawala anakuwa juu ya katiba huku kapewa madaraka yote unategemea nn kwann asiswage watu katiba Ina mruhusu.
Eti Kinga ya kutoshtakiwa then utegemee maendeleo,haki, demokrasia, katiba inawaruhusu hata kuongoza watu Kama Mali yao binafsi
 

Kwa upinzani huu mtasubiri miaka 25 kutoka sasa
Kipimo tukutane Oktoba 25 sanduku la kura likitoa majibu
 
Mmawia. Tume huru haiombwi lazima watu waingie kitaa. La sivyo zitaendelea kudumu fikra za Magu
 
Yaani tumtoe ikulu Magufuli halafu tumuweke nani, Mbowe, Lissu, Msigwa au Nyarandu? hii itakuwa wendawazimu kabisa kwa sasa tuacheni, mkajipange vizuri tukutane 2025.
 
Hongera sana kwa Malawi, unaona wenzetu wanavyotupita? Jamani tumwadhibu Nduli huyu anaturudisha nyuma sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…