Malawi wameweza, Tanzania tunafuatia

Tanzania haikuwahi kuwa na vyama vingi, ile ni geresha tuu.
 

Mkuu Mawia, nakukubali kwa jinsi unavyojitahidi kujijengea matumaini mithili ya mfa maji.

Unajua ukweli kwamba vyama vya upinzani Tanzania, hadi sasa, vinaongozwa na viongozi wanasiasa wachanga, wachumia tumbo na wanaharakati. Badala ya kujijenga kwa jamii ya wapiga kura, wanafanya hivyo kwa jamii yenye uwezo wa kutumia TEHAMA. Kutwa watajinasibu mitandao ya kijamii au kutumia vyombo vya habari. Wanayongoea huko zaidi ni ya kinadharia, kama siasa za zamani za kutoa ahadi hewa, au kutafuta huruma ya wasomaji.

Hivyo basi kulinganisha Malawi na Tanzania ni sawa na kulinganisha chui na paka. Serikali ya CCM imegusa kila sehemu ya maendeleo ya mpiga kura kwa vitendo, jambo ambalo viongozi wengi wa Bara la Afrika na hata nchi zote zinazoendelea, wameshindwa.

Naamini hapo ulipo, japo unashutumu kwa minajiri ya kujifariji, Tanzania ya leo siyo ya jana.
• Wanao, kama unao, wanasoma bure;
• Iwapo una gari lako mwenyewe barabara zimeboreshwa;
• Kama uko Chuo, mkopo unapata kwa wakati;
• Wewe ni mjasiriamali, basu husumbuliwi hovyo kana zamani; nk
 
Eti wachumia tumbo, [emoji23][emoji23][emoji23] unaweza kutuwekea ushahidi wa kiongozi wa upinzani aliye wahi kushitakiwa kwa ufisadi wa mali za umma?

Je ni mafisadi wangapi wa ccm wametuhumiwa na kufikishwa mahakamani kwa ufisadi kama siyo mamia?

Viongozi wenu wanakamatwa na silaha za maangamizi, risasi kibao, huoni aibu? Wacha kuendekeza njaa
 
Kawadanganye mazuzu wenzako wa lumumba
 
Unajijua kuwa unaendekeza njaa kwa kutetea maovu kwa kujifanya huoni wachumia tumbo waliop ndani ya ccm
Kuna vyombo vya Dola vinavyoshughulikia wasiotii sheria, na kamwe sijatetea na sintotetea watu wa aina hiyo kama unavyofanya wewe. Kwangu maisha yangu na ya familia ndiyo muhimu, hao wanasiasa wanaganga njaa zao.

Kudanganywa na wanasiasa kwa ahadi hewa, kama iilivyokuwa zamani, kumepitwa na wakati.
 
Tumedanganywa sana kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne, wewe unafaidika na nini kama siyo kulijaza tumbo lako tu huku ukiwaacha ndugu zako waendelee kuwa ombaomba?
 
Tumedanganywa sana kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne, wewe unafaidika na nini kama siyo kulijaza tumbo lako tu huku ukiwaacha ndugu zako waendelee kuwa ombaomba?
Suluhisho lake?
 
Tunabadili walio tutawala kwa hicho kipindi na kuwapa kijiti wengine watuonyeshe uwezo na uadilifu wao wa kutuongoza.

Imefika wakati kama umeshindwa basi kaa pembeni wenzako wenye uwezo wafanye kilicho kushinda maana hakuna mwenye leseni ya kuitala nchi.
Suluhisho lake?
 
Tunabadili walio tutawala kwa hicho kipindi na kuwapa kijiti wengine watuonyeshe uwezo na uadilifu wao wa kutuongoza.

Nakubaliana na wewe. Unadhani au unaamini nani mwenye uwezo na uadilifu wa kutuongoza ili tumpambe mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu badala ya kuendeleza shutuma na lawama kwa uongozi uliopo madarakani?
 
Nakubaliana na wewe. Unadhani au unaamini nani mwenye uwezo na uadilifu wa kutuongoza ili tumpambe mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu badala ya kuendeleza shutuma na lawama kwa uongozi uliopo madarakani?
Vyama vipo na viongozi wao ni bora kabisa, sioni haja ya kumtaja mmoja mmoja hiyo ni kazi ya wapiga kura, wekeni uwanja ulio sawa wa kufanya siasa muwaachie wananchi waamue
 
Vyama vipo na viongozi wao ni bora kabisa, sioni haja ya kumtaja mmoja mmoja hiyo ni kazi ya wapiga kura, wekeni uwanja ulio sawa wa kufanya siasa muwaachie wananchi waamue

Kwamba Vyama vipo na viongozi wao ni bora kabisa kwa Sera zipi na vigezo vipi, vya ubora, walivyo navyo hao viongozi wake?

Kuhuhusu Tume Huru ya Uchaguzi, Katiba ya JMT Ibara ya 74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa
na Rais:-
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama yaRufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtuanayeshika, aliyewahi kushika au anayestahilikuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.[/I]


Je, ni kifungu kipi kinacho inyima uhuru hiyo Tume?
 
Yes
Thus aliweka mifumo ya kidikteta inayotuumiza leo
Ndio maana marafiki zake walikuwa akina Mobutu seseko, Milton Obote, Kamuzu Banda na wengine madikiteta wa kila aina including akina Fidel Castrol. Pia kutokana na umaskini na kwa kuogopa kunyimwa misaada akaja na sera za ujamaa za kutofungamana na upande wowote lakini kimsingi jamaa alikuwa dikiteta na aliwapenda madikiteta kama Urusi, korea na china. Waaraby hawakuwa na pesa hakujenga urafiki nao.
 
Mkuu mbona una hasira kama za mkizi. Unakataa tamaa kirahisi hivyo kuna jambo kweli utajuja ufanikiwe maishani?
 
Mageuzi yapi sawa haya licha yake nani unaona anafaa hata uminzani kama karibia wote wamekaa kikunguru. Nani yupo credible?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…